Simba SC Yapokea Kipigo Kutoka kwa Raja Casablanca

Klabu ya Simba ambayo inaongozwa na kocha mkuu Robertinho imepokea kichapo cha mabao 3-1 dhidi ya Raja Casablanca kwenye mchezo wao wa marudiano hapo jana.

 

Simba SC Yapokea Kipigo Kutoka kwa Raja Casablanca

Mchezo huo ulipigwa majira ya saa 7:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki huku Simba wakimkosa beki wao Mohamed Hussein ambaye alikuwa na kadi tatu mfululizo za njano kwenye michuano hiyo.

Mechi ya kwanza vijana wa Msimbazi walichezea kichapo cha mabao 3-0, na jana licha ya kufungwa matatu walifanikiwa kupata bao 1 la kufutia machozi ambalo lilitupiwa kimyani na Jean Baleke.

Simba SC Yapokea Kipigo Kutoka kwa Raja Casablanca

Baada ya kupoteza mchezo huo mnyama amesalia nafasi ile ile ya pili akiwa na pointi zake 9, wakati kwa upande wa Raja Casablanca yeye bado ndiye kinara wa kundi hilo akiwa na pointi zake 16.

 

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.