Wakala wa mchezaji nyota wa Real Madrid Marco Asensio amethibitisha kuwa klabu za Arsenal na Ac Milan kuvutiwa na huduma ya mchezaji huyo kwenye vikosi vyao ili kuongeza nguvu kwenye msimu ujao.
Marco Asensio kwenye kipindi cha alitumia muda wake wa mapumziko ya kimataifa nchini Italia na ilisababisha kuzuka kwa tetesi kuwa kuna uwezekano wa yeye kuhamia kwenye dimba la Stadio Meazza.
Ac Milan wana uhusiano mzuri na klabu ya Real Madrid kufuatia usajiri wa Brahim Diaz na Theo Hernandez. Kulingana na taarifa zilizopo, wakala wa mchezaji Asensio amekutana na viongozi wa Milan wiki chache zilizopita, na wakala wa mchezaji huyo amethibitisha hilo.
“Tunajivunia Milan kuvutiwa nasi, Rossoneri ni chaguo hata kama kuna offa kutoka kwenye vilabu vya ligi ya kuu ya uingereza, ikiwepo Arsenal. Tuko tayari kuchambua sehemu sahihi.” Wakala wa Marco Asensio.
Milan kwa sasa wanataka kuboressha kikosi chao kwa kuongeza mshambuliji wa pembeni na kiungo wa katikati kwenye majira ya kiangazi. Mkataba wa Asensio na klabu ya Madrid unaisha mwaka 2023, na inasemekana kuwa Madrid wameshampa mkataba mpya wenye thamani €5milioni kwa mwaka, lakini bado hajaweka saini mpaka sasa.
Asensio kwa sasa anaangalia uwezekano wa Kylian Mbappe, ikiwa atatua kwenye klabu hiyo kama mchezaji huru mwisho wa msimu. Kama ikitokea, basi na yeye anaweza kutafuta mahala pengine pakwenda kupata nafasi ya kucheza zaidi.
3500 NI YAKO UKIJIUNGA TU MERIDIANBET!
Una nafasi ya kupata bonasi ya shilingi 3500 kwa ajili ya kuanza safari yako ya kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.