Bale: Kustaafu 2022? Mguu Nje, Mguu Ndani.

Mwaka 2022 unaweza kuwa ni mwaka ambao utatawaliwa na matukio makubwa kwenye ulimwengu wa soka. Gareth Bale anaweza kuwa miongoni mwa matukio ya mwaka 2022.

Miongoni mwa matukio makubwa yanayotegemewa kwa mwaka 2022, mojawapo ni Kombe la Dunia kule nchini Qatar. Ufaransa atafanikiwa kutetea ubingwa? Akishindwa, bingwa atakua nani? Vipi kuhusu CR7, atafanikiwa kucheza mashindano hayo au ndio mwisho wake kuipeperusha bendera ya Ureno?

Baada ya misimu ya soka kumalizika kwa ngazi ya vilabu, usajili wa dirisha kubwa utakuwa wazi. Huku kuna kujua hatma ya Kylian Mbappe, Paul Pogba, Erling Haaland na pengine, Lewandowski. Nani anakwenda wapi? 2022 itatuambia.

Kwa Gareth Bale kuna vitu viwili vitaamua 2022 unakuwa ni mwaka wa aina gani kwake. Inaripotiwa kuwa, endapo Wales watafanikiwa kufuzu kucheza Kombe la Dunia, Gareth ataendelea kucheza soka. Kama Wales watashindwa kutoboa hatua ya mtoano ambayo wapo kwa sasa, tutegemee mchezaji huyo kustaafu soka baada ya msimu huu kuisha.

Anaumri wa miaka 32 tu kwa sasa. Mkataba wake na Real Madrid unatamatika mwishoni mwa msimu huu. Huyu ni nahodha wa timu ya Taifa ya Wales ambayo, taifa hili halijawahi kucheza Kombe la Dunia toka mwaka 1958. Endapo watafanikiwa kuipata tiketi ya kwenda Qatar, Bale anafikiria kuchezea moja wapo ya timu hizi: Cardiff City au Swansea.

Bale: Kustaafu 2022? Mguu Nje, Mguu Ndani.

Lengo la Gareth kwenda kwenye mojawapo ya timu hizi, ni kujiweka fit kwa ajili ya Kombe la Dunia na hivyo, atajiunga nazo kwa mkataba wa muda mfupi. Tofauti na hapa, atastaafu soka 2022.


TENGENEZA FAIDA NA ZEUS ANCIENT FORTUNES

Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe