Waswahili husema, “majuto ni mjukuu” neno “Ninge..” huja baada ya matokeo kuonekana. Edinson Cavani, athibitisha uhalisia wa maneno haya.

Mkataba wa awali wa Cavani na Manchester United ulikua unatamatika mwishoni mwa msimu ulioisha. Hata hivyo, aliyekua kocha wa United wakati ule (Ole Gunnar Solskjaer) alifanikiwa kumshawishi nyota huyo kusalia Old Trafford kwa msimu mmoja zaidi.

Wakati mazungumzo ya Ole na Edi yanaendelea, Cavani hakufahamu kama United inampango wa kumsajili Cristiano Ronaldo. Alikubaliana na mipango ya Ole akiamini atakua na nafasi kubwa kikosini hapo. Fumba na kufumbua, siku ya mwisho ya dirisha la usajili, CR7 akatua Old Trafford akitokea Juventus. Hapa ndipo Edi alipoanza kuyaona majuto yake.

Cavani, Cavani: “Kama Ningelijua Mapema..”, Meridianbet

Anaheshimika kwa uwezo wake wa kuongea ukweli kama ulivyo, bila kupindisha maneno. Edinson ameeleza wazi kuwa, kama angelijua mapema mpango wa United kumsajili CR7, asingelikuwepo klabuni hapo wakati huu. Angeondoka mwishoni mwa msimu ulioisha.

Sio kwa sababu asingetaka kucheza pamoja na Ronaldo hapana, lakini angeondoka klabuni hapo ili kumpisha nyota huyo na kuendeleza mipango yake mingine ya soka nje ya United.


TENGENEZA FAIDA NA ZEUS ANCIENT FORTUNES

Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa