Shughuli za Mateu Alemany na Jordi Cruyff zimekuwa zikiangaziwa kwa jicho maalum la vyombo vya habari huko Barcelona katika miezi ya hivi karibuni.

Mkurugenzi wa Soka na Katibu wa Ufundi amekuwa kwenye shamra shamra, safari hii wakielekea London.

Sport wanasema walikuwa katika mji mkuu wa Uingereza kuzungumza na Chelsea kuhusu madili ya wachezaji kadhaa tofauti.

La kwanza ni lile ambalo Barcelona wanavutiwa nalo zaidi. Ni Beki Cesar Azpilicueta, ambaye amekuwa akizua gumzo tangu mwanzo wa mwaka. Barcelona wanadaiwa kutaka kumleta Camp Nou. Hivi majuzi kandarasi yake iliongezwa na Chelsea, lakini inasemekana ana chaguo la kuondoka kwa bei nzuri.

Mchezaji wa pili kwenye ajenda ana wasifu sawa, ni beki wa kushoto wa Celta Vigo, Javi Galan, ambaye amekuwa akihusishwa na Barcelona.

Chaguo la tatu litakuwa na athari kubwa zaidi kwenye mfumo wa Barcelona na ujenzi wa kikosi. Inasemekana kuwa Barcelona wanataka kuleta jina kubwa katika nambari tisa kwa msimu ujao na Romelu Lukaku atakuwa kwenye harakati za majira ya joto.

Mabosi wa Barcelona Watimba London

Inaonekana kuwa changamoto kwa  Barcelona kulipa kiasi kama hicho cha pauni milioni 97.5 alichonunuliwa na Chelsea kwa msimu uliopita wa joto, lakini anaweza kuwa mbadala wa mkopo ikiwa Barcelona itashindwa kumpata Robert Lewandowski.


TENGENEZA FAIDA NA ZEUS ANCIENT FORTUNES

Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.

CHEZA HAPA


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa