Dani Alves Bado Amekasirishwa na Kusimamishwa Kwake

Dani Alves amekasirishwa na uamuzi huo uliopelekea kusimamishwa kwake kwa mchezo mmoja zaidi.

Mkongwe huyo wa Barcelona alionesha kiwango bora dhidi ya Atletico Madrid mwishoni mwa juma, akifunga na kutoa asisti wakati Barcelona wakiondoka na ushindi wa 4-2.

Lakini Dani Alves alipokea kadi nyukundu dakika 20 za mwisho, ambayo ilikuwa na utata kwa mchezo wake dhidi ya Yannick Carrasco, mwenyewe akisisitiza kuwa ni ajali.

Rekodi ya picha ya video zinaonyesha uamuzi ulikuwa sahihi, na kwa sababu Alves hakuwa na nafasi ya kuwania mpira wakati wa tukio hilo, amepigwa marufuku kwa michezo miwili.

Dani Alves Bado Amekasirishwa na Kusimamishwa Kwake
Dani Alves akionekana kuwa azimio lake halikuwa kuwania mpira.

Sheria za RFEF zinasema adhabu ya kawaida ya kufungiwa kwa mchezo mmoja kwa faulo isiyo ya hatari, iongezwe na mchezo ikiwa hakuna nia ya kuwania mpira.

Uamuzi huo unamaanisha kuwa Alves atakosa mechi ya debi ya Catalonia dhidi ya Espanyol wikendi hii na pambano dhidi ya Valencia, huku pia akikosa mechi ya Ligi ya Europa dhidi ya Napoli kutokana na kutosajiliwa kwenye michuano hiyo.

Habari hii haijawa nzuri kwake, na amenukuliwa akisema: “Ni ujinga kwamba mchezaji mwenza wa taaluma hii atafanya uharibifu kwa mwingine kwa makusudi. Tunacheza mchezo wa hatari na ajali hutokea, na sio lazima kwenda mbali zaidi. Hata hivyo, Carrasco, nisamehe tena kwa ajali.”


KASINO YA MTANDAONI: EMOTICOINS SABABU YA KUVUNA ZAIDI.

Haijawahi kuwa rahisi hivi kwenye safari yako ya kuvuna mkwanja, kasino maridhawa ya meridianbettz inakuletea mchezo wa Emoticoins unaokupa nafasi ya kufanya safari yako kuwa rahisi zaidi. Wakati ni wako nafasi ni yako na Emoticoins.

senegal, Senegal Mabingwa AFCON 2021., Meridianbet

CHEZA HAPA.

Acha ujumbe