EPL Itaendelea Licha ya COVID19 Kusambaa.

Baada ya matokeo ya vipimo vya COVID19 kuonesha kuwa hali sio shwari nchini Uingereza, uongozi wa EPL umesema hauna mpango wa kusitisha michezo inayoendelea msimu huu.

Kumekuwa na hali ya sintofahamu kuhusu muendelezo wa michezo ya EPL baada ya vilabu mbalimbali kuathirika na COVID19, michezo kadhaa ilighairishwa na baadhi ya vilabu kuzuiliwa kuingiza mashabiki viwanjani.

Kutokana na sintofahamu hiyo, Premier League imetoa tamko kuwa “hatujajadili kusimamisha msimu.

“Ligi itaendelea kuzingatia utaratibu wa kujilinda na COVID19 ili kuwezesha michezo kuendelea kama ilivyopangwa, taratibu hizi zinaendelea kusimamiwa na serikali.

“Kwa kuzingatia usalama wa wachezaji na wafanyakazi wote kwenye vilabu, ligi inaungana na vilabu katika kutekeleza taratibu zilizowekwa.”

Licha ya kwamba EPL itaendelea, mashabiki hawatoruhusiwa tena kuingia viwanjani kama sehemu ya kujilinda na COVID19. Ni Liverpool na Everton pekee ndio vilabu vilivyokuwa vinaweza kupokea mashabiki 2,000 na sasa vilabu hivyo havitoruhusiwa kufanya hivyo tena.


VUNA SHEA YAKO YA 230,000,000TSH NA UFURAHIE MSIMU HUU WA SIKUKUU!!!

Kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, jiwekee nafasi ya kupata shea yako ya 230,000,000Tsh kupitia mchezo wa Secret Santa. Hakika hutojutia kufurahia msimu huu wa sikukuu ukiwa katika nyumba ya mabingwa ya Meridiabet. Unasubiri nini?

SOMA ZAIDI

18 Komentara

    Corona ituache jamani

    Jibu

    Du corona ni janga kubwa

    Jibu

    Dar colona sio poa

    Jibu

    Coronavirus sio poa

    Jibu

    Maamuzi waliyosema ni sahihii kabisa

    Jibu

    Ni sawa ila wachukue tahadhari

    Jibu

    Hii ni hatari sana lakini Corona imeshaonyesha kuwa ni ugonjwa ambao tunatakiwa kuishi nao

    Jibu

    Wachukue tahadhari

    Jibu

    Safi sana nimependa msimamo wao

    Jibu

    Habari njema ila tahadhari ni muhimu maana corona haiwezi kuisha leo

    Jibu

    Corona inazidi kuwa kikwazo jamn

    Jibu

    Corona sio poa

    Jibu

    Corona noma sana

    Jibu

    Bora tu

    Jibu

    Covid inaleta hasara

    Jibu

    Hawaja chelew tahadhari muhim

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.