Baada ya kuwepo kwa hali ya sintofahamu muda mfupi baada ya vilabu kadhaa vya EPL kutowaachia wachezaji kucheza timu za Taifa, madhara yake yameonekana.
Takribani wachezaji 8 wanaocheza EPL, watakosekana viwanjani kwa siku 5. Hii ni baada ya shirikisho la soka nchini Brazili kuitaka Fifa kutekeleza sheria ya kuwafungia wachezaji ambao hawakuitikia wito wa kuitumikia timu yao ya Taifa.
Ederson, Alisson, Gabriel Jesus, Fred, Fabinho, Firmino, Thiago Silva na Rafinha ni wachezaji ambao walipaswa kuitumikia Brazili lakini kutokana na vilabu vyao kutowaruhusu wachezaji hao kwenda Brazili, sasa wachezaji hawa watakaa nje ya uwanja kwa siku 5.
Inaripotiwa kuwa tayari Fifa imeshavitaarifu vilabu hivi (Man United, Man City, Liverpool, Chelsea na Leeds United) kuhusu hali ya wachezaji hao na hivyo vilabu vinapaswa kufikiria mipango mingine ya kuendelea bila wachezaji hawa kwa siku 5.
Hili huenda likawa ni pigo kubwa kwa United ambao wanamkosa Scot McTominay (majeruhi) na sasa Fred katika safu yao ya kiungo. Kwa Man City, watamkosa kipa wao namba 1.
Meridianbet inakuletea ushindi kwenye kiganjani kwako, unafurahia radha halisi ya burudani ya kasino mtandaoni na tabasamu la ushindi.



[email protected]
Du pole yao