Harry Kane Apata Majeraha

Mshambuliaji wa klabu ya Fc Bayern Munich na nahodha wa timu ya taifa ya Uingereza Harry Kane imetaarifiwa anasumbuliwa na majeraha ya misuli ya nyama za paja katika mchezo wa jana wa ligi kuu ya Ujerumani dhidi ya Borussia Dortmund.

Harry Kane alishindwa kumaliza mchezo wa De Klassiker jana ambapo alitolewa baada ya kupata majeraha na kuingia mkongwe Thomas Muller, Baada ya mchezo jana kocha Vicent Kompany alieleza kua jeraha la mshambuliaji huyo halionekani kama jeraha baya sana.harry kaneBaada ya kufanyiwa vipimo na taarifa kutoka leo na kueleza mshambuliaji huyo anasmbuliwa na misuli ya nyama za paja, Huku ikiwa haijaelezwa atakaa nje ya uwanja kwa muda gani lakini kikawaida majeraha ya aina hiyo hua yanachukua wiki kadhaa mpaka miezi itategemea tu na ukubwa wa tatizo.

Mshambuliaji Harry Kane ambaye atakaa nje ya uwanja kwa wiki kadhaa ni wazi litakua pigo kubwa kwa klabu ya Bayern Munich, Kwani mchezaji huyo amekua na kiwango na kufunga magoli ambayo yameiweka kalbu ya Bayern Munich kileleni mwa msimamo wa Bundesliga mpaka sasa lakini pia kiujumla amekua mchezaji muhimu kwenye eneo la ushambuliaji namna amekua akiunganisha timu kwenye eneo hilo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.