Mchezaji wa Borussia Dortmund anayegonga vichwa vya habari duniani kote, Jardon Sancho amefikiana makubaliano binafsi na klabu ya Manchester United dakika kadhaa zilizopita na sasa wanasubiri kutoka Borussia Dortmund.

Sancho amekuwa katika wakati mzuri misimu miwili iliyopita na inaonekana kuwa Manchester United wanahitaji sana huduma ya mchezaji huyo pale Old Trafford.

Taarifa kutoka Ujerumani zinadai kuwa Jadon Sancho na wakala wake hawana tatizo lolote na Jadon yupo tayari kujiunga United.

Kinachosubiriwa sasa ni Manchester United kuzungumza na Borussia Dortmund ili wakubaliane kuhusu dau la kumng’oa mchezaji huyo, huku BVB wakitaka Euro Milioni 95.

Borussia Dortmund wanasema wapo tayari kwa timu yoyote ambayo itafikia dau la euro milioni 95 kama United watashindwa kufikia bei hiyo. Jadon sasa anasubiri tu United wafanya yao kisha ajiunge United mpaka Juni 2026.


WEKA PESA KUPITIA DUKANI MERIDIANBET!

Chukua namba yako ya akaunti na kiasi cha pesa unachotaka kuweka, sogea kwenye duka lolote la Meridianbet lililo karibu nawe utasaidiwa kuweka pesa.

Weka Pesa Meridianbet

WEKA PESA

5 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa