Katika umri 33, hakuna mtu ambaye angemlaumu Santiago Carzola kama angeamua kustaafu. Hiyo ni kutokana na misukosuko aliyopitia ndani ya miaka mitatu nyuma.

Ila Carzola yeye alikuwa na fikra tofauti kabisa na dunia, aliamini anaweza kurudi na walau kucheza mchezo mmoja wa mwisho ili aweze kuwaga mashabiki waliolifia soka.

Santiago Carzola
Santiago Carzola

Mkasa mzima uliaanza October 2016. Carzola alipata majeraha kwenye kifundo cha mguu. Mwanzo ilidhaniwa ni tatizo la kawaida hadi alipofanyiwa vipimo na kugundulika ilikuwa ni suala zito.

Sehemu ya kano (tendon) kwenye kifundo chake cha mguu ilikuwa imechimbika kwa sentimeta nane. Madaktari walikiri kuwa Hakukuwa na uwezekano wa kutibu jeraha bila kupata kano mbadala kutoka sehemu nyingine ya mwili wake.

Santiago Carzola

Hivo walizamika kukata sehemu ya nyama ya mkono wake ili waweze kulitibu jeraha lake. Carzola akapoteza tatoo ya mwanae mpendwa aliyokuwa ameichora mkononi mwake.

Mwaka 2017 alifanyiwa ‘operation 8’ tofauti katika harakati za kumpatia matibabu ya kifundo chake cha mguu.

Madaktari walimuambia itakuwa bahati sana kama ataweza kunyanyuka na kutembea kwa miguu yake, achilia mbali kuweza kucheza mpira.

Mkataba wake na Arsenal ukamalizika December 2018, wakaachana naye.

Ila madaktari sio Mungu bwana. Carzola alinyanyuka tena, muda ukaenda, ndoto za kurudi uwanjani zikarejea tena.

Akàanza kutafta form kwa kufanya mazoezi na timu ya vijana ya Alaves. Dirisha la Majira ya joto timu yake ya utotoni Villareal ikamsajili.

Santiago Carzola
Santiago
Baada ya siku 636 za kuuguza majeraha akavaa jezi tena na kuingia uwanjani. Ilikuwa Mchezo wa kirafiki kati ya Villareal na Heracles, alipotokea nje.

Baada ya hapo haikuwa tena stori ya Carzola kulemaa. Perfomance yake la liga iliwakumbusha benchi la ufundi la Hispania kuwa bado yupo.

May 2019 akaitwa timu ya taifa tena. Baada ya siku 1302 akunusa harufu ya jezi ya timu ya taifa tena.

Mchezo wa Spain na Malta wahispaniola walimuona yule Carzola waliyomzoea.. alicheza dakika 59.

Wakati anatoka mashabiki walisimama kumpigia makofi kumpongeza.


BONASI YA 50% KILA SIKU KATIKA KASINO ZA EVOPLAY HAPA MERIDIANBET.

Meridianbet na Evoplay Kasino wanakupa bonasi ya 50% ya kiasi utakachoweka katika akaunti yako leo. Unasubiri nini ni wakati wa kupiga pesa sasa na Mabingwa.

tuchel, Tuchel :Tuna Bahati Tottenham Wametusaidia Kazi., Meridianbet

SOMA ZAIDI

3 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa