Bayern Munich yamsajili Omar Richards kuwa beki wa timu hiyo baada ya kuachana na David Alaba mapema mwezi huu. Richards amesajiliwa kama mchezaji huru kutoka Reading ya Uingereza.

Omar anaenda Munich kwenda kurithi mikoba ya Alaba ambaye atajiunga na Madrid saa chache zijazo. Akiwa na Munich, Alaba amefanikiwa kufanya mambo makubwa sana ikiwemo,:

🇩🇪 Bundesliga (x10)
🇩🇪 DFB-Pokal (x6)
🇩🇪 DFL-Supercup (x5)
🇪🇺 Champions League (x2)
🇪🇺 UEFA Super Cup (x2)
🌎 FIFA World Club Cup (x2)

Omar amefanikiwa kucheza michezo 100 akiwa na Reading toka mwaka 2017 na baada ya kusajiliwa, Richards alionesha furaha yake kwa kudai kuwa ni ndoto yake kucheza pale Germany.

“Uhamisho wangu kwenda Bayern ni heshima kubwa sana kwangu, ni ndoto kuwa kweli”, alisema Richards.

Je, Omar Richards atafanikiwa kuvaa viatu vya nyota huyu mkubwa mwenye sifa kubwa na kipaji maridhawa kabisa?


BONASI YA 50% KILA SIKU KATIKA KASINO ZA EVOPLAY HAPA MERIDIANBET.

Meridianbet na Evoplay Kasino wanakupa bonasi ya 50% ya kiasi utakachoweka katika akaunti yako leo. Unasubiri nini ni wakati wa kupiga pesa sasa na Mabingwa.

tuchel, Tuchel :Tuna Bahati Tottenham Wametusaidia Kazi., Meridianbet

SOMA ZAIDI

4 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa