Kabwili post yako inasikitisha Ila kama unataka kuondoka basi ondoka hapo ulipo kwa maana hilo ni jini ulilo lihifadhi kwenye kwenye mfuko wako.
Kabwili
Kabwili
Ukiniuliza kawaida nilimuona Kabwil mkubwa kwenye milingoti ya Yanga kabla ya Rostand, Metacha, Kindoki na hata Shikalo. Kwani Yanga ilipokwama chini ya kocha George Lwandamina ulinzi wa nguzo tatu ulibaki chini yake na waliishi salama kama mtu anaekwepa ukimwi kwa kutumia kinga.
Katika kipindi hicho Kabwili alithibitisha sehemu ya ubora wake kwa kucheza Derby na mechi za kadhaa za kimataifa ikiwemo dhidi ya Zanaco toka Zambia.
Baadae ubovu wa kindoki langoni chini ya Mwinyi Zahera bado Kabwli alitosha kuibeba Yanga kwenye michezo lukuki.

Naamini Yanga walikuwa na muda sahihi wa kumpromote huyu kijana kwa kumpa hope huenda leo wangeishi wakiwa salama lango kuliko mashaka waliyonayo juu ya Metacha na Shikalo wakiwa hawana jibu hadi sasa nani anaweza kuwa usalama wa uhakika.

Turudi nyuma kidogo kwenye ukwei Yanga na Simba haziamini kwenye kukuza na kujenga imani na vijana wao wenyewe, mimi naamini Metacha hakuwa mkubwa zaidi ya Kabwili kabla ya kuja Yanga, kwa idadi ya mashindano na mechi walizocheza na hata timu aliyotoka

Metacha alitoka mbao ambayo aliiacha ilipo leo na Kabwili alionesha ubora wake kwenye mahitaji ya msingi ya Yanga na taifa kwa ujuma hasa kwenye AFCON U17 pale Gabon.

Kabwili

Sisemi metacha hafai Yanga ila kabla ya Metacha walipaswa kuwaza kuhusu Kabwili.

Namaliza kwa kusema, Ondoka Kabwili Yanga sio kiatu chako, usipo nisikiliza utakuwa kama kipa wa zamani wa Simba Sc Muhagama Kelvin alisota benchi akipokea wenzake waje kucheza mpaka akaitwa Radio ya timu

Usiondokee Instagram, ondokea moyoni, Yanga ipo milele usipokuwa mchezaji utakuja kuwa shabiki ukimaliza soka


MAANA KAMILI YA USHINDI KATIKA KASINO ZA MERIDIANBETI NI PAMOJA NA MCHEZO WA PANDA PANDA.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Panda Panda na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

Gomes, Gomes : Sitafanya Usajili wa Kutisha., Meridianbet

CHEZA HAPA

2 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa