Kieran Trippier Afungiwa kutojihusisha na Masuala ya Mpira wa Miguu Baada ya kuvunja Sheria za FA kufuatia kujihusisha na Masuala ya Ubashiri (Betting). Beki huyo wa zamani wa Tottenham anayekipiga Atletico Madrid amefungiwa kujihusisha na shughuli za mpira kwa kukutwa na makosa ya kuvunja sheria za michezo kwa kubashiri.
Kwa mujibu wa Taarifa ya FA, Trippier amekutana na kifungo hicho kwa kukutwa na kosa la kuvujisha habari ya ndani kuhusu uhamisho wake kutoka Tottenham kwenda Atletico Julai 2019, ambapo habari hizo zilitumika kufanyiwa ubashiri juu ya uhamisho wa mchezaji huyo.
Trippier amepewa hadi kufikia Mei 18 kuwa amekata rufaa, nyota huyo wa kimataifa wa England mwenye umri wa miaka 29 sasa anacheza mpira wake nchini Uhispania, hivyo FA italazimika kuomba FIFA kutekeleza kifungo hicho cha kutojihusisha na maswala ya soka. Trippier inaripotiwa kuwa amekiuka sheria mbili kama zile za mchezaji wa zamani wa Chelsea na Liverpool Daniel Sturridge. Ikumbukwe Sturridge alifungiwa miezi minne na alipigwa faini ya Pauni 150,000.
Daniel
Spurs miss him at Right Back #MeridianbetTZ
Furahav
Mmh hatorudia kubashiri.
Rehema dickson
Ndo pole kwake
Salma
Bora apewe adhabu iwe funzo kwa wachezaji wengine
Neema juma
Akishajua kosa lake hatorudia tena
Njiku
Yupo poa sanaa
Gabriel
Kwel wezetu sheria zao nzur
felister
kafungiwa kwa muda gani…?