Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Uingereza, Manchester City wako kwenye moto wao msimu huu ukiwa unaelekea ukingoni, wakiwa wamepania kujikusanyia mataji yote 4 wanayoshiriki msimu huu. Licha ya ukweli kuwa Man City wapo kwenye fomu nzuri lakini bado ushindani kwenye michuano yote ni mkubwa, makosa kidogo tu kwenye EPL yanaweza kuwafanya wakamshuhudia Liverpool wakinyakua taji hilo.
Baada ya Man City kushinda taji la EFL, huu unaweza kuwa msimu wao wa neema na kuvunja historia kama wakikusanya mataji yote wakiwa wameanza na EFL kisha wakabamba EPL, UCL na FA Cup.
Kuelekea Fainali ya FA Cup
Man City wamelazimika kuchomoka na ushindi mwembamba wa 1-0 dhidi ya Brighton na kuweza kupenya kuingia fainali za Kombe la FA. Goli la mapema kabisa dakika ya 4 lilitosha kuwahakikishia Man City ushindi huku wakikosana kosana na wapinzani wao Brighton. Man City wanatarajia kukutana na mmoja kati ya Watford na Wolveshampton kwenye fainali ya kombe hilo Mei 18.
Wasi wasi wa Guardiola
Guardiola anatazama ushindani mkubwa uliopo na uzoefu wa gemu walizocheza na kuwa na wasiwasi kama kweli wanaweza kushinda mataji manne msimu huu.
“hakuna klabu iliyoweza kufanya hivyo (kushinda mataji manne), kwa nini tunaweza kushinda? Ni kama haiwezekani hivi kushinda kila kitu, huo ndiyo ukweli…. Ninafurahia tumeingia fainali, tunaongeza wiki moja mbele kwenye msimu wetu.” -Guardiola
Ushindiani uliopo kwa michuano yote ni mkubwa hivyo matumaini yaliyopo bado yanaweza kukumbana na vikwazo kama sio kukwama kabisa, Guardiola anasema licha ya kuwa mabo yanabadilika kila siku ikiwa ni pamoja na kupata majeruhi kila siku anaamini kuwa bado wana nafasi ya kupambana na watafanya hivyo.


Furahav
Man city wako vizuri.