Donny Van de Beek, Muholanzi asiye na maneno mengi ila uwezo wake uwanjani ni uthibitisho wa kiwango safi cha kucheza soka. Baada ya kutua Man United, mambo yamebadilika kidogo.
Man United ilimsajili Van de Beek katika dirisha la majira ya kiangazi kwa dau la pauni milioni 40 akitokea Ajax alipoanzia maisha yake ya soka na kujitengenezea jina kubwa kwenye ulimwengu wa soka.
Akiwa United, Donny amecheza michezo michache akianzia benchi kwenye michezo mingi ya EPL. Licha ya kutopata nafasi nyingi za kuonesha kipaji chake akiwa United, nafasi chache alizopata alizitumia vyema kuonesha yeye ni mchezaji wa aina gani.
Wachambuzi na wapenzi wa soka maeneo mbalimbali duniani wamekuwa wakimtupia maneno kocha wa Man United – Ole Gunnar Solskjaer kwa kushindwa kumtumia vizuri mchezaji huyu licha ya kuwa na kiwango kikubwa kuwazidi wachezaji wanaotumika sana.
Solskjaer alishasema “Donny atakuwa na jukumu kubwa ndani ya United na muda wake utafika.” Kauli ya Ole inaungwa mkono na Van de Beek ambaye amekiri ni suala la muda tu na anaimani muda huo unafika ndani ya muda mchache ujao.
“Sipendi kulisema hili ila ni kweli, ningependa kupata muda zaidi wa kucheza. Ninajisikia vizuri kuwa kwenye klabu kubwa. Nilipokelewa vizuri na nilisaidiwa na kila mtu.” alijibu Donny baada ya kuulizwa na NOS kuhusu hali yake ndani ya kikosi cha Man United.
“Mimi ni mtu mwenye subira, lakini unakwenda pale ukiwa na lengo la kucheza mara kwa mara. Pia ninadhani kwa kila muda ambao nimecheza, nimeonesha ni kitu gani ninaweza kukiongeza kwenye timu.
“Solskjaer amesema nini kuhusu mimi? Ninatakiwa kuwa na subira, lakini pia ninatakiwa kuendelea kufanya ninachokifanya.
“Ameona ninamchango mkubwa ninapokuwa uwanjani. Muda wangu utafika na wakati hizo fursa zinapokuja, ninatakiwa kuzitumia ipasavyo.”
Katika mechi 3 za Ligi ya Mabingwa, Van de Beek anawastani mkubwa (92%) wa kupiga pasi kuwazidi viungo wengine wa Man United – Matic (89.4%), Pogba (85.5%), Fred (84.1%), McTominay (83%) na Fernandes (73.3%).
Jaribu sasa hapa Meridianbet. Ukiacha ukweli kuwa itakupa burudani maridadi, bado inakuhakikishia ushindi mkubwa. Kazi kwako kukusanya ushindi!



Khadija
Asante kwa makala
Lydia Emmanuel Magoti
Safii Sana Van uwezo unajionyesha mpambanaji kilakitu kina kwenda namipango kajisemea Van
Fatina mfingi
Safi San van kujiamni ndo kitu muhim kwenye maish!
Elika
Safi sana kijana yuko vizuri,kijana yuko makini
Magdalena
Kijana mwenye kujituma uwanjani
Tatu
Kijana anajiamini sana
Saupha mohamed
Safi sana van uko ni kujiamini
Angelina
Goodnews
Mwajumah
Safi sana kijana
Carolyn
Subira ni nzuri sana
Adelta
Safi Sana van umejuwa kutufurahisha
Mashabiki
Dorophina
Van de beek yupo vizuri sana anajua nini anafanya
Sabrina
Nakubali van de beek
felister
vizurii
Janeflora malisa
Safi
Ester jackson
Good news
Rahma
Asante kwa makalq
Shani
Muda utaongea
Zeiyana
Kila kitu kina kwenda na mda wake ukiangalia kwenye maisha ya mpira kila siku wanaibuka wachezaji wapya mwenye uwezo kupita yeye kikubwa hangalie mda wake sasa mashabiki wake wanatamani kuona uwezo wake kwa mala nyengine akiwa clabuni hapo
Povel
Van de beek ni kwl wakati wakuchez united ukifikah tu
Issa
Van de beek ataleta mapinduz united