Klabu ya Simba sports Club inayoshiriki ligi kuu ya nchini Tanzania NBC Premier League imepanga kuwashukuru mashabiki wake kwenye mchezo wake wa mwisho dhidi ya Mtibwa Sugar FC.

Simba inakwenda kucheza mchezo wake wa mwisho kwenye uwanja wake wa nyumbani, pia kuna matukio mawili makubwa ambayo wanakwenda kuwayafanya kwenye mchezo huo wa kesho dhidi ya mtibwa sugar.

Simba

Moja wapo ni kumuaga beki wao aliyemaliza muda wake Pascal Wawa na lingine ambalo ndio la muhimu ni uongozi wa klabu ya Simba kuwashukuru na kuwaaga mashabiki kwa kuendelea kujitoa kwa ajiri ya klabu yao.


Pia mtendaji mkuu wa klabu hiyo Babra Gonzalez, atatumia fursa hiyo kwa kuzunguka majukwaa yote ambayo wanasimba watakayo kaa kwa ajiri ya kutoa shukrani na kuwaaga maashabiki, Uongozi wa simba utatumia mchezo huo kutoa zawadi kwa shabiki bora wa msimu ambapo atakabidhiwa jersey ya klabu hiyo.

Simba inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa NBC premier league, ambapo bingwa wa ligi tayari ameshajurikana na sasa wanakwenda kukamilisha idadi ya michezo

Simba msimu huu anamaliza msimu pasipo kuwa na kombe lolote, huku mchezo wa mwisho akisafiri kwenda jijini mbeya kumalizana na Mbeya Kwanza FC.


ALIYA’S WISHES

Bila shaka unatamani ushindi mkubwa, vipi kuhusu kujaribu Sloti hii ya Aliya’s Wishes? jaribu ushinde sasa.Kasino ya Mtandaoni

CHEZA SASA


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa