Miaka 39 iliyopita pale kwenye udongo wenye upako wa soka nchini Brazil, mji wa Porto Alegre ndipo anatokea fundi wa mpira mmoja wakuitwa Ronaldo de Assis Moreira ‘Ronaldinho Gaucho’ dunia ya soka na watu wa kupenda soka la burudani kama Mimi tunamfahamu vizuri huyu bwana.

Sio sisi tu kutoka mitaa mbalimbali duniani bali hata wale wahafidhina wa Real Madrid waitwao Madridista wanamuheshimu mno, ile mitaa ya Concha Espina mpaka Cibeles pale Madrid walimuheshimu mnyama akiwa na uzi wa Barca, Dinho alifungamagoli mawili pale Bernabeu na uwanja ukampa Heshima kwa kusimama uwanja mzima (standing oviation,) ukimtoa Diego Maradona na Iniesta ni Dinho tu alipewa heshma hiyo pale Bernabeu.
Dinho alikua ni mbunifu mno, alipiga kila aina ya chenga, kila aina ya ujuzi, pale Barcelona walimpa nafasi ya winga, walimpa nafasi kama straika muda mwingine ila namba 10 ilikuwa inampendeza sana, alifunga ndoa na mabeki jumlisha na makipa.
Ila unyama wake kwenye ile staili ya flip flap au elasticoau snake bite ilikuwa staili ya Roberto Rivelino, fundi mmoja wa mpira kutoka hapo hapo Brazil ila Dinho aliiona kupitia vipande vya video, wengi walijaribu wakashindwa ila Dinho aliiweza, chenga ilikuwa inataka kasi ya miguu na ujuzi wa daraja la kwanza, ukijaribu ovyo utavunja miguu.

Dinho baada ya kuipatia hiyo chenga basi Rivelino akaishia kutabasamu, kinda anapanda ndege kutoka Brazil kwenda Paris anahama nayo mpaka Nou Camp, huku kote mabeki walitamani kutoa ushuhuda juu ya pigo hilo la snake bite
Wachezaji wenzake wa Barcelona wanakwambia hakuna kiumbe chochote kilichowahi kuwa na utulivu mbele ya msitu wa mabeki kama Gaucho, anacheza huku anacheka, mashabiki pembeni nao wanafurahi, huo ndio ulikua uwezo wa Gaucho.


Furahav
Gaucho alikuwa noma.
farida ahmadi
Habari njema Sana
Issa
Dinho afai