Rais wa klabu ya Barcelona Joan Laporta amesema winga wa klabu hiyo raia wa Ufaransa Ousmane Dembele hayupo kwenye mipango ya kuuzwa na klabu hiyo.

Winga Dembele amekua akihusishwa kuandoka ndsani ya klabu ya Barcelona kwa muda mrefu sasa, Lakini Rais Laporta amesema mchezaji huyo hayupo kwenye mipango ya kuzwa na timu hiyo na wanapanga utaratibu wa kukaa nae chini ili kuzungumzia suala la mkataba mpya ili aweze kusalia kwenye viunga vya Camp Nou.dembeleTaarifa za ndani za klabu ya Fc Barcelona zinaeleza kua mchezaji huyo ni miongoni mwa wachezaji waliotakiwa kuwekwa sokoni, Lakini ujiowa kocha wasasa klabuni hapo Xavi Hernandez ulikwamisha mpango huo kwani alionesha nia ya dhati yakutaka winga huyo kusalia ndani ya Barcelona.

Rais Laporta amekanusha uvumi wa kua Dembele anaondoka klabuni hapo na kuelekea klabu ya PSG na kusisitiza kua winga huyo yupo kwenye mipango ya klabu hiyo na hawana mpango wa kumuuza mchezaji zaidi ataendelea kusalia klabuni hapo.dembeleWinga Ousmane Dembele amekua kwenye kiwango bora sana tangu kuja kwa kocha mpya wa klabu hiyo Xavi na kusababisha klabu hiyo kuvutiwa na mchezaji huyo na kutaka aendelee kusalia klabuni hapo. Klabu ya Barcelona itafanya mazungumzo na mchezaji huyo miezi sita inayofuata ili kumuongezea mkataba aendelee kusalia klabuni hapo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa