Mshambuliaji wa klabu ya PSG Neymar Jr atakosekana katika mcheza ujao wa Ufaransa wa Ufaransa kutoka na majeraha ambayo ameyapata mchezaji huyo.

Staa huyo anasumbuliwa na tatizo la enka tangu mchezo wa kwanza wa kombe la dunia dhidi ya timu ya taifa ya Serbia, Jeraha hilo limekua likimsumbua mpaka wakati huu na kumfanya kupata maumivu mara kwa mara.neymarKocha wa klabu ya PSG amesema kua Neymar atakosekana katika mchezo ujao wa kombe la Ufaransa dhidi ya klabu ya Chateauroux, Na hiyo ni kutokana na mchezaji huyo kutokuonekana katika mazoezi ya klabu hiyo leo Alhamisi.

Neymar ambaye alipata kadi mbili za njano mbili katika mchezo wao wa kwanza wa ligi kuu ya Ufaransa baada ya michuano ya kombe la dunia dhidi ya Strasbooug, Kadi ambazo zilimfanya akose mchezo wa ligi kuu dhidi ya klabu ya Lens ambao ndio mchezo wao wao kwanza kupoteza msimu huu.neymarKocha wa klabu hiyo Christopher Galtier baada ya kutoa taarifa ya kukosekana kwa staa huyo katika mchezo unaofuta, Lakini pia ameeleza kua staa mwingine wa timu hiyo Lionel Messi ambaye amerejea mazoezini jana hatakuepo pia kwenye mchezo huo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa