Kiungo wa timu ya taifa ya Hispania na klabu ya Atletico de Madrid Koke amefunguka kua kocha Luis Enrique aliekua kocha wa timu ya taifa ya Hispania ambaye ameachia kazi hiyo rasmi anaweza kua mrithi sahihi wa Diego Simeone pale Atletico.
Luis Enrique ameachia ngazi rasmi siku ya jana ya kuinoa timu ya taifa ya Hispania baada ya kutolewa kwenye michuano ya kombe la dunia siku ya jumanne na timu ya taifa ya Morocco katika mchezo wa 16 bora.Kocha huyo baada ya kuingoza Hispania maarufu kama La Roja kwa takribani miaka minne aliamua kuachana na timu hiyo baada ya kushindwa kuifikisha hatua za mbali kwenye michuano ya kombe la dunia huko nchini Qatar.
Koke ambaye alikua kwenye kikosi cha Enrique ambacho kilitupwa nje ya michuano ya kombe la dunia siku ya jumanne anaamini kocha huyo licha ya kua na falsafa tofauti na Simeone lakini anaweza kua mbadala sahihi wa Muargentina huyo aliedumu klabuni hapo kw muda mrefu.
Akihojiwa na wanahabari Koke alifunguka “Enrique ni kocha mzuri sana, Ana falsafa za tofauti na tulizokua nazo pale lakini kwanini hapana. Ni wazi aliongeza kitu kwa kila mtu, vyombo vya habari, Wachezaji na klabu kwasababu anataka kiwango kizuri, Nafikiri yuko Vizuri”Kiungo huyo ameonesha kwa kiwango gani anamkubali kocha na anatamani siku moja avae viatu vya Diego Simeone pale Atletico de Madrid, Kipindi ambacho Muargentina huyo anazungumzwa sana kuondoka klabuni hapo baada ya kukaa kw amuda mrefu.