Klabu ya Real Madrid imepoteza mchezo wake wa pili katika ligi kuu ya Hispania leo baada ya kukubali kipigo cha mabao mawili kwa moja dhidi ya Villarreal.

Klabu ya Villarreal imeweza kuchukua alama zote tatu katika dimba lake la nyumbani dhidi ya klabu ya Real Madrid baada ya kuifunga mabao mawili kwa moja katika mchezo huo uliopigwa katika dimba la Estadio de le Ceramica.real madridReal Madrid ambayo ilianza mchezo huo ikiwa haina mchezaji raia wa Hispania kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa akwa klabu hiyo miaka 121 iliyopita, Ilijikuta ikiangukia pua baada ya kuzidiwa mbinu na vijana wa Quigue Setien na kuruhusu kufungwa mchezo huo.

Mabao ya Yeremy Pinno na Gerard Moreno yalitosha kuwapa Villarreal alama tatu muhimu huku goli la kufutia machozi la vijana wa Carlo Ancelotti likifungwa na Karim Benzema. Mabingwa hao watetezi wataendelea kusalia katika nafasi ya pili na alama zao 38.real madridKlabu ya Villarreal wao wameendeleza ubabe wao dhidi ya klabu ya Real Madrid wa kutokukubali kufungwa na klabu hiyo katika uwanja wao wa nyumbani. Mara ya mwisho Los Blancos kupata matokeo dhidi ya Villarreal katika uwanja wao wa nyumbani ilikua mwaka 2017 hivi imepita takribani miaka sita sasa.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa