Manchester United Yatakata Kombe la Dunia

Klabu ya Manchester United inayoshiriki ligi kuu ya Uingereza imetakata kwenye michuano ya kombe la dunia siku ya jana katika michezo miwili tofauti.

Klabu hiyo imetakata baada ya wachezaji wake kufanya vizuri siku ya jana katika michezo miwili tofauti kati ta Brazil dhidi ya Uswisi na ule ulipigwa usiku kati ya timu ya taifa ya Ureno dhidi ya timu ya Uruguay.manchester unitedWachezaji wa Manchester United Bruno Fernandes na Carlos Casemiro jan walifanikiwa kuzisaidia timu zao kupata alama tatu muhimu na kufuzu hatua ya 16 bora baada ya timu ya taifa ya Ufaransa kufanya hivo hapo kabla.

 

Carlos Casemiro alifanikiwa kufunga bao pekee lililoiwezesha Brazil kupata ushindi dhidi ya timu ya taifa ya Uswisi katika mchezo ambao ulionekana kua mgumu zaidi. Huku Bruno Fernandes nae akiwa kwenye ubora mkubwa alifanikiwa kufunga mabao mawili ambayo yaliisaidia timu yake kupata ushindi dhidi ya Uruguay usiku wa jana.manchester unitedBaada ya mchezo huo wachezaji hao wa klabu ya Manchster United walikabidhiwa tuzo zao za mchezaji bora wa mechi huku Casemiro akiwa mchezaji bora wa mechi kati ya Brazil dhidi ya Uswisi na Bruno Fernandes yeye akiwa mchezaji bora katika mchezo wa timu ya taifa ya Ureno dhidi ya Uruguay.

 

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.