Hasira za Kocha Mkuu wa Simba, Didier Gomes kwa sasa zipo katika kubeba makombe mawili ya ndani ambayo anashindania sambamba na watani zao wa jadi, Yanga.
Gomes amepania kumaliza msimu huu kwa kutetea mataji yao waliyoyatwaa msimu uliopita ambayo ni Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho la Azam.
Tayari ndani ya Ligi Kuu Bara, Simba ndiyo vinara wakiwa na pointi 61 baada ya kucheza mechi 25. Mbio zao za kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika zilikwama Mei 22 baada ya kutolewa na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini kwa jumla ya mabao 4-3 ambayo Simba ilifunga.
Gomes amesema: “Bado nina deni ambalo natakiwa kulilipa Simba pamoja na kuweka alama kwenye mashindano haya (CAF) kwa kufika hatua hii tuliyofika kwa mara ya pili mfululizo.
.
“Sasa nguvu zetu tunakwenda kuziweka katika mashindano ya ndani na kuchukua kila kombe lililopo mbele yetu kutokana na ubora wa kikosi kilivyo naona tuna kila sababu ya kufanya hivyo”
Msimu huu ikitokea Simba ikabeba tena mataji hayo, itakuwa ni msimu wa nne mfululizo Yanga inakosa ubingwa wa Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho la Azam.
BONASI YA 50% KILA SIKU KATIKA KASINO ZA EVOPLAY HAPA MERIDIANBET.
Meridianbet na Evoplay Kasino wanakupa bonasi ya 50% ya kiasi utakachoweka katika akaunti yako leo. Unasubiri nini ni wakati wa kupiga pesa sasa na Mabingwa.
Kila la kheri simba
Kila la kheri simba