Hatma ya Ousmane Dembele inaweza kuamuliwa hivi karibuni, kwa mujibu wa raisi wa Barcelona Joan Laporta.
Katika utambulisho wa Luuk de Jong kama nyota wa mwisho kusainiwa Barcelona, Laporta ameamua kugusia hatma ya staa ya mazungumzo ya mkataba wa Dembele.
Nyota huyu wa Ufaransa kwa sasa yupo nje ya uwanja akiuguza jeraha, na amepewa jezi namba saba pale Camp Nou.
Laporta anasema amehakikishiwa kuwa mkutano na mawakala wa staa huyu unaandaliwa ili kuweka sawa suala lake la mkataba mpya.

Raisi huyu hana wasiwasi na uhusiano wao na Ousmane Dembele, anaamini kuwa anafurahia kuwepo Barca, na anahisi kupendwa na klabu, hivyo angependa suala hilo liendelee.
Ousmane Dembele alikuwa na mchango mkubwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa kwenye michuano ya EURO 2020.
Akiwa chini ya Ronald Koeman msimu uliopita, Dembele alichangia magoli sita kwenye mechi 30 za ligi alizocheza.
Barcelona kwa sasa wanapambana na msimu mgumu kwa sasa, baada ya kuwapoteza mastaa wao wakubwa Lionel Messi na Antoine Griezmann, hivyo wanajitahidi kuhakikisha wanasalia wachezaji wao muhimu.
Meridianbet inakuletea ushindi kwenye kiganjani kwako, unafurahia radha halisi ya burudani ya kasino mtandaoni na tabasamu la ushindi.


