Fowadi wa Paris Saint-Germain Kylian Mbappe ni anaripotiwa kuwa yupo tayari kukubali punguzo la mshahara ili kujiunga na Real Madrid msimu huu.

Staa huyo bado hana uhakika na uwepo wake Parc des Princes wakati mkataba wake wa sasa ukimalizika Juni 30.

Mbappe anahusishwa zaidi na klabu ya Real Madrid, licha ya ripoti moja ikidai kuwa mabingwa hawa wa La Liga wana matumaini ya nafasi yao ya kumsajili staa huyu wa Ufaransa majira haya ya joto.

Kwa mujibu wa Marca, mpango wa Mbappe ni kujiunga na Real Madrid majira haya ya joto na yupo tayari kukubali punguzo la mshahara wake wa sasa ili kukamilisha safari yake kwenda Santiago Bernabeu.

Mbappe: Tetesi za Soka Barani Ulaya.

Ripoti inaongeza kuwa Mfaransa huyu amekuwa wazi juu ya nia yake ya kusalia PSG, lakini bado hana imini na ‘mradi wa michezo’ wa klabu hiyo na sasa anatarajia kutafuta changamoto mpya na Los Blancos.

Mbappe amekuwa bora mbele ya lango la upinzani msimu huu 2021-22, alifunga mara 35 na kutoa asisti 23, katika mechi 43 alizoichezea PSG katika mashindano yote.


 

TENGENEZA FAIDA NA ZEUS ANCIENT FORTUNES

Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa