Mchezaji wa Manchester United na Timu ya Taifa ya Uingereza, Jesse Lingard, bado anasoma upepo kabla ya kuamua hatma yake ndani ya kikosi hicho.
Imeripotiwa kuwa, Lingard amegoma kusaini mkataba mpya wa kuendelea kubaki United licha ya uongozi wa klabu hiyo kumtaka mchezaji huyo kusalia kikosini hapo.

Inasemekana, suala linalomvuta nyuma Jesse, ni uwepo wa wachezaji wawili – Jadon Sancho na Cristiano Ronaldo. Usajili wa wachezaji hawa, ni dhahiri umeongeza ushindani wa namba kwenye kikosi cha Solsksjaer na hivyo, ni sahihi kwa Lingard kuangalia nafasi yake ya muda mrefu kwenye kikosi cha The Red Devils.
Mkataba wa JLings na United unatamatika mwishoni mwa msimu huu na kumekuwa na uhusishwaji wa baadhi ya vilabu kunyatia mchezaji huyu. FC Barcelona na AC Milan ni miongoni mwa vilabu vinavyohusishwa na Jesse.
Fanya wiki yako iwe ya kuvutia zaidi, tunaelekea Los Angeles kutengeneza mkwanja na kasino maridhawa ya LA Rouge kutoka katika kasino za mtandaoni za meridianbettz, Fursa ya kufurahi huku unajaza pochi yako.

CHEZA HAPA

