Man United Wameweka X Ofa ya Sevilla.

Anthony Martial ameweka wazi lengo lake la kutaka kuondoka Old Trafford. Amesikilizwa na ataruhusiwa kuondoka Man United, kama timu inayomtaka itafikia vigezo vya kuachiwa.

Barcelona na Juventus ni miongoni mwa vilabu vinavyohusishwa na Martial lakini, taarifa zinasema mchezaji huyu ameichagua Sevilla akiamini ndio sehemu ambayo atapata nafasi ya kucheza mara kwa mara.

Awali, kocha wa muda wa Man United, Ralf Rangnick alithibitisha matakwa ya Martial na kuongeza kuwa, kufikia muda ule (kabla ya mchezo dhidi ya Newcastle United), klabu haikuwa imepokea ofa yeyote kwa mchezaji huyo. Akasisitiza, endapo hali itaendelea kuwa hivyo, Martial hanabudi kuendelea kuwepo kwenye viunga vya Carrington Complex.

Anthony Martial

Fumba na kufumbua, Sevilla wamepeleka ofa yao ya kwanza kwa United ili kumsajili Martial mapema mwezi Januari, 2022. Inasemekana ofa ya Sevilla imekataliwa na United kwasababu imelenga kumsajili kwa mkopo wa miezi 6 na kulipa nusu ya mshahara wake tu. Hakuna kipengele kitakachowafunga Sevilla kumsajili mchezaji huyo moja kwa moja.

Man United wamewafungia pazia Sevilla kwa kile kinachodaiwa kuwa, vigogo hawa wa Uingereza na Ulaya, wanataka timu inayomuhitaji Martial, imlipe mshahara wake wote pamoja na kulipia ada ya usajili wa mkopo. Tofauti na hapo, mshambuliaji huyo ataendelea kubaki United ambapo amebakiza mkataba wa miaka mitatu (mpaka 2024).


KUWA BINGWA MSIMU HUU WA SIKUKUU NA OCEAN CALL

Nani hapendi kuwa bingwa na kujishindia mkwanja wa kusahato kuelekea katika sikukuu wiki hii. Mchezo wa Ocean Call kutoka kasino maridhawa za meridianbettz unakupa kila sababu ya kuifanya siku kuu yako kuwa ya kuvutia zaidi.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe