Klabu ya Man Utd itawakosa nyota wake nne kwenye mchezo wa kesho dhidi ya klabu Everton kwenye dimba la Goodison Park kocha wa klabu hiyo athibitisha.
Man Utd inatafuta alama ambazo zitamfanya aweze kujihakikishia kuwa anamaliza ligi akiwa kwenye nafasi nne za juu ili afanikiwe kucheza ligi ya mabingwa ulaya kwa msimu ujao, kwaiyo mchezo dhidi ya everton ambayo nayo inataka kujihakikishia inabaki ligi kuu ni muhimu kwa vilabu vyote viwili.
Rangnick amethibitisha hilo kwenye mkutano wake na waandishi wa habari kwamba Edinson Cavani, Scott McTominay, Luke Shaw na Raphael Varane hawatakuwepo kwenye mchezo wa kesho.
Alex Telles, Victor Lindelof na Nemanja Matic wanatarajiwa kuanza huku kwenye nafasi ya ushambuliaji ikiongozwa na Cristiano Ronaldo ambaye anatarajiwa kuanza baada ya kukosekana kwenye mchezo uliopita.
Klabu ya Man Utd imekuwa na matatizo ya nafasi za ulinzi kwenye msimu, kukosekana kwa Shaw na Varane ni pigo kubwa kwa klabu hiyo, lakini kurejea kwa Ronaldo kutaongeza hamasa kwa wachezaji na timu nzima.
Maana halisi ya ushindi mkubwa unaipata katika kasino ya mtandaoni ya Aviator kutoka meridianbettz. Andaa kapu la ushindi wa mkwanja na beti kibao za BUREEE.