Luke Shaw Kufanyiwa Upasuaji wa Kuondoa Vyuma Mguuni

Mlinzi wa klabu ya Manchester United Luke Shaw ataukosa mchezo wa keso dhidi ya Everton na anatarajiwa kuwa nje kwa wiki huku akijiandaa kufanyiwa upasuaji mdogo wa kuondoa vipande vya chuma .

Luke Shaw aliondolewa kwenye mchezo wa wikiendi iliyopita wa ligi kuu ya Uingereza dhidi ya Leicester City baada ya kusumbuliwa ka maumivi kwenye mguu wake ambao aliwai kuumia kabla na kuwekewa vyuma.

Luke Shaw
Luke Shaw

Mchezaji huyo wa kimataifa wa uingereza alipata majeraha hayo ya kuvunjika mara mbili kwenye mguu wake kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa ulaya dhidi ya PSV Eindhoven mwaka 2015, na  alifanyiwa uapsuaji na kuweka vyuma ili kutibu tatizo hilo.

Kocha wa muda wa klabu ya Manchester United  Ralf Rangnick ameweka wazi  kwamba mlinzi wake wa kushoto kwa sasa anajianda kufanyiwa upasuaji mdogo siku ya jumamosi ili kuondoa vyuma alivyowekewa, na atakuwa njee ya uwanja kwa takribani wiki mbili mpaka tatu.

“Luke Shaw bado majeruhi, tulimuondoa kipindi cha kwanza dhidi ya Leicester City, alikuwa na tatizo la mguu wake ambao alifanyiwa upasuaji mwaka 2015. Daktari aliniambia kuwa wameamua kumuondoa vyuma  walivyomuweka kwenye mguu wake na kesho ndio kazi itaanza na atakuwa nje kwa wiki mbili hadi tatu.” Ralf Rangnick aliwaambia waandishi


VUNA MKWANJA NA AVIATOR

Maana halisi ya ushindi mkubwa unaipata katika kasino ya mtandaoni ya Aviator kutoka meridianbettz. Andaa kapu la ushindi wa mkwanja na beti kibao za BUREEE.

 

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

SOMA ZAIDI

Acha ujumbe