Klabu ya Manchester United ipo kwenye mkakati wa kuanzisha sera mpya ya kupunguza mishahara ndani ya klabu hiyo ambayo imepewa jina la Cristiano Ronaldo.

Klabu hiyo inataka kuanzisha sera hiyo ili kupunguza matumizi ndani ya klabu hiyo ambayo imekua ikitumia kiasi kikubwa cha fedha kwa muda mrefu. Man United inataka kuweka utaratibu wa kuweka mishahara ya chini na kima cha juu kimepangwa kiwe paundi laki mbili kwa wiki.Manchester UnitedKlabu ya Manchester United kwa muda mrefu imekua ikisifika kama timu ambayo imekua ikilipa vizuri zaidi mishahara ya wachezaji wake na hii ilitokana na klabu hiyo kufanya vibaya kwa muda mrefu, Hivo jambo pekee ambalo klabu hiyo ilikua inatumia kuvutia wachezaji ni mishahara mikubwa.

Klabu hiyo chini ya Mtendaji mkuu Jorh Murtough akishirikiana na kocha wa klabu hiyo Erik Ten Hag inaelezwa wamekubaliana sera hiyo ianze kutekelezwa klabuni hapo kwakua itawasaidia kupunguza matumizi makubwa, Vilevile itaifanya klabu hiyo kua na uchumi imara kwa muda mrefu.Manchester UnitedBaada ya taarifa hiyo kutoka baadhi ya wadau na mashabiki mbalimbali wa klabu ya Manchester United wameoneshwa kutofurahishwa na sera hiyo, Kwani wengi wanaamini kuweka ukomo wa mishahara mwishi paundi laki mbili kwa wiki itawanyima klabu hiyo kupata wachezaji wakubwa wenye ubora wa dunia.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa