Hebu tujiulize kitu, Vipi kuhusu kejeli alizotupiwa tarehe 20 January 2001? Dunia nzima imesimama siku ile, watu wanautazama urefu wa Diego Corrales wanamuuliza Mayweather unaenda kufanya nini. Wanaufikiria uzito wa ngumi za Corrales wanamuambia Mayweather unaenda kupoteza muda tu, wanayatazama maisha ya Diego wanamuambia Maywethwer unaenda kupigwa wewe. Ila laiti kama wangejua MAYWEATHERameshuka kama nabii wa Sodoma na moto wa Gomora, wasingezungumza.
Mayweather anaitazama picha ya bibi yake, alafu anavaa gloves zake kisha anamtazama mjomba wake mzee Roger Mayweather ambaye ni kocha wake, anamwambia, “ninakwenda kumpiga huyu.” Anapanda ulingoni.

Hilo lilikuwa ni pambano la ubingwa wa super-featherweight lililopigwa ndani ya GM Grand Arena, Las Vegas, kati ya Fyold Mayweather na Diego Corrales. Wote walikuja hapa wakiwa hawajapoteza pambano hata moja. Lilikuwa pambano la kwanza la Diego Corrales baada ya kutoka jela. Alihukumiwa kwenda jela mwaka mmoja baada ya kupatikana na hatia ya kumpiga mke wake.
Licha ya kuzidiwa uzoefu na mpinzani wake,Mayweather alisema “ninajua yeye ni bingwa wa dunia, ila hilo sitajali, ninakwenda kumpiga kama alivompiga mke wake, na nitamkumbusha kuwa siku nyingine anatakiwa kuwaheshimu wanawake.”
Wengi waliamini Mayweather anajipa moyo tu. Mayweather hakubishana nao, alisubiri kuzikosoa fikra zao ulingoni. Walipofika ulingoni, Mayweather alishinda kila round. Baada ya Corrales kudondoka kwa mara ya tano, kocha wake alitupa taulo ulingoni, na siku hiyo Mayweather alijitangaza kuwa bingwa mpya wa dunia wa uzito wa super-featherweight. Hakuruhusu ngumi zaidi ya tisa zimpate ndani ya round moja.
Historia ya Floyd Joy Mayweather Junior inaanzia pale.


Tahiya
Mpambanaji asiyekata tamaa aliamini kuwa anaweza na kwer amejipatia mafanikio makubwa sana
SADICK
Ni boxer mzuri, binafsi huwa sivutiwi sana na mbinu zake za upiganaji #meridianbettz
Zeiyana iddi
Mayweather alijiamini sana ndio maana akua na of na mwisho wa siku akaweza..!
Emmy cleopa
Ahsante meridian kwa habar za burudan
Gabriel
Jamaa anahistoria nzur kwenye michezo ya ngumi 🥊
David pere
Huyu jamaa akisikia harufu ya pesa anachanganyikiwa kabisa Ndio maana anatudi kupigana
mwakalosi
huyu man money atastaafu pasipo kupigwa
Antony Luseno
Kastaafu masumbwi kwa kutimiza ndoto zake
Furahav
Huyu kwel kidume ila hasiombe kupigana na mike Tyson atadedi.
Rehema
Huyu jamaa ni mpambanaji mzr asiekata tamaa kwenye mchezo wa ngumi
Mwanahamisi
Ni boxer nzuri anakubalika
Tatu
Mayweather ni mpambanaji asiyekata tamaa
Theonestina
Namkubar Sana uyo jamaa
Ester
Yuko vizuri sana hata watu wengi wanamkubali kwa upambanaji wake
dorophina
Ni mpiganaji mzuri na ajawahi kupigwa katika mapambano yake
Magdalena
Kukata tamaa n mwiko katika kuusaka ubigwa ndicho alichokifanya Mayweather
#meridianbet
Amani
Yuko vizuri sana hata watu wengi wanamkubali kwa upambanaji wake#meridianbettz
Povel
My weather yupo vzr thanks meridian kwa information
Lydia Emmanuel Magoti
Mayweather yupo vizuri kwenye pambano langumi anajua jama uyo
Neema juma
Mpambanajiii yuko makinii kinomaaa
Lydia Emmanuel Magoti
Yupo vizuri anajua mpambanaji uyo
Mariam mtandama
Yupo vizur
lombo
mambo ya masumbwi
winfrida
namkubali sana mayweather
frank patrick
Araf Conor analilia kupigwa tena na Money Man…
Khadija
namkubali sana mayweather no mpiganaji asiyekubali kushindwa#meridianbettz
Mwajuma
Ni mpiganaji mzuri asiekata tamaa
Hidaya Mohammed
Asante sana meridianbett kwa taharifa hz
aisha
my weather yuko vizuri na pia sio mtu wa kukata tamaa
felister
namchompendea uyu jamaa hajui kukataa tamaa
Ernest
Huyu jamaa ngumi jiwe
Isaya massawe
Naamini atafikia ndoto zake maana anafanya vizuri sana akuna asie mkubali
Issa suddy
Maywether ngumi jiwe
nasra
Huyu Jamaa anaonaga mbali
Hope mwaikuka
Jamaa ni unstoppable
Samiah
Jamaa yupo vzr
Rehema Dickson
Jamaa ngumi chuma uyu sio wa pole pole
Samira
Ni bonge moja la mpambanaji ulingoni
Agness
Mayweather ni bonge la star
Elika
Yuko vizur myweather na anajiamini