Novak Djokovic Aipinga Chanjo ya COVID-19

Mkali wa mchezo wa tenisi duniani, Novak Djokovic amesema kwamba yeye atakwenda kinyume na suala la wao kulazimishwa kupatiwa chanjo ya ugonjwa wa Corona ambao umeibuka ili kushiriki michuano yao!

“Binafsi sikubaliani na suala la chanjo. Sipendi mtu anilazimishe mimi kufanya jambo hilo ili niweze kusafiri kuelekea kwenye michuano ya tenisi kwa wachezaji wanaohusika.” Alisema hayo bingwa huyo wa tenisi duniani siku ya Jumapili.

Staa huyo wa Serbia alikuwa akizungumza hayo kutokea nchini Hispania, ambako amefungiwa kutoka nje yeye pamoja na familia yake, katika mkutano wa video alioufanya kupitia Facebook kwa ajili ya Orthodox Easter.

“Sisi wachezaji tutatakiwa kusafiri. Ninadhani hiyo ni changamoto namba moja,” alinena mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32.

Mkali wa mchezo wa tenisi duniani, Novak Djokovic amesema kwamba yeye atakwenda kinyume na suala la wao kulazimishwa kupatiwa chanjo ya ugonjwa wa Corona ambao umeibuka ili kushiriki michuano yao!

“Endapo chanjo italazimishwa unadhani ni nini kitatokea? Nitatakiwa kuchukua maamuzi magumu,” alisema maamuzi hayo yatakuwa ni juu ya kukubali ama kukataa chanjo hiyo.

“Haya ni mawazo yangu kwa wakati huu. Sijui kama nitayabadilisha tena siku zijazo!”

Kwa sasa hakuna chanjo ya kutukinga na ugonjwa huo wa Corona ambao mpaka leo umeua takribani zaidi ya watu 165,000 duniani kote, ingawa maabara mbalimbali duniani zinajaribu kuendelea kutafuta dawa ya ugonjwa huu.

Kama ambavyo imekuwa na kwa wengine wote wanaojihusisha na michezo duniani, mapema mwezi Machi michezo ya tenisi ilisimamishwa kwa muda kutokana na janga hili, kwa sasa inatarajiwa kuwa Michuano ya Tenisi ya ATP pamoja na ile ya WTA Tours itaendelea kuahirishwa mpaka ifikapo katikati ya mwezi Julai kwa makadirio ya siku za karibuni ambapo pia Wimbledon imefutwa kwa mara ya kwanza tangu kipindi cha Vita ya Pili ya Dunia itokee.

Djokovic anakadiria kuwa michuano hiyo ya kidunia haitoanza upya kabla ya mwezi Septemba na Oktoba mwaka huu.

“Msimu utaanza rasmi wakati kila mtu atakapokuwa na uhakika wa asilimia 100 kwamba watu wanaweza kurudi tena kutazama michezo yote, kwamba hakutakuwa na hatari ya maambukizi tena, kwamba watu watakuwa wakiweza kujikinga dhidi ya virusi hivyo na hii yote itachukua muda sana.”

Alisema kwamba inawezekana kabisa michuano ikafanyikia sehemu moja ama katika eneo moja litakalopendekezwa.

22 Komentara

    safi vzr sana. kinga ni muhimu sana .asante kwa taarifa #meridianbetttz

    Jibu

    Chanjo ni bora kuliko tiba

    Jibu

    huyu jamaa kachanganyikiwa nadhani maana huwezi kataa tiba katika janga kama hili

    Jibu

    yuko sahih

    Jibu

    Kama imethibishwa vzur chanjo n bora zaid sio ya kupinga

    Jibu

    sio mbaya kila mtu ana maamuzi yake

    Jibu

    Ni Jambo zuri maana chanzo Ni bora kuliko tiba Asante meridian kwa habar za kimichezo

    Jibu

    Kama sijamuelewa hivi

    Jibu

    Hili swala la chanjo kizungumkuti sana, kila mtu anawaza lake kichwani.

    Jibu

    kila mtu ana maamuzi yake ana haki ya kukataa

    Jibu

    Kuna sababu ya yeye kupinga itakua hiyo chanjo inamadhara

    Jibu

    kafanya la maana kujipa kinga

    Jibu

    Kinga ni bora kuliko tiba ,asipinge kabla hajajuwa dawa ya corona.

    Jibu

    Siyo mbaya maana kila mtu anamaamuzi yake.

    Jibu

    Djokovic ni international figure hapaswi kupingana na Sayansi ya tiba bila ushahidi kuwa ina madhara. Angechagua kukaa kimya. 🙏🙏🙏🙏# meridian kwa makala nzuri

    Jibu

    Anahaki ya kusikilizwa

    Jibu

    Djokovic ana hoja la msingi #meridianbettz

    Jibu

    Asante meridian kwa habar

    Jibu

    Huyu jamaa huwaga Mtata sana#Meridianbettz

    Jibu

    Vzr mana zingine sio bali sumu.

    Jibu

    Novak tunatakiwa tujilinde na covid 19

    Jibu

    Vizuri lakini kila mtu ana huwamuzi wake yeye Kama yeye kaona Haina mahana kwake

    Jibu

Acha ujumbe