Ole Gunnar ameweka wazi mtazamo wake kuwa Man City ndiyo timu bora zaidi Uingereza. Ole Gunnar amesema hivyo kufuatia klabu hizi kukutana kwenye nusu fainali ya Kombe la EFL.
Manchester United waliwalaza chali Colchester United kwa bao 3 bila wakimalizana na mechi yao ya mwisho kwenye robo fainali.
Droo ya nusu fainali mewakutanisha miamaba wa Manchester na Ligi Kuu ya Uingereza City na United. Inakumbukwa debi iliyopita ya miamba hawa, United waliweza kuwalaza chali vijana wa Pep Guardiola, hii ni fursa ya Man City kurekebisha makosa.
Hata hivyo, licha ya kuchapa Man City kwenye mech iliyopita, Ole Gunnar anasalimu amri kuwa klabu ya Manchester City chini ya Meneja Pep Guardiola ndiyo timu bora zaidi Uingereza.
“Tuna waheshimu sana, na kama nilivyozungumza baada ya debi iliyopita, kwa maoni yangu wao ni timu bora zaidi Uingereza.” -Ole Gunnar
Hata hivyo, bado Ole Gunnar ana matarajio kuwa kikosi chake kitafanya vyema kwenye nusu fainali.
Povel
Habar njema