Ralf Rangnick Aruhusu Wachezaji Kusemana.

Wakati Manchester United wakiwa katika ubora wa chini kuliko matarijio ya wengi, kocha wa muda, Ralf Rangnick anaendelea kutafuta mbinu sahihi kwa wachezaji wake.

Kumekuwa na ripoti kadha wa kadha zinazohusu mahusiano mabovu baina ya wachezaji ndani ya Manchester United. Hii ni hali inayopelekea mgawanyiko kati yao na kwa sehemu kubwa, inawaathiri uwanjani kama timu.

Katika kuliweka hili wazi, Cristiano Ronaldo alisema wazi alipozungumza na kituo cha habari cha Sky Sports ambapo alisema;

Ili msimu huu uwe wa mafanikio, baadhi ya wachezaji wenzake wanapaswa kubadilisha mitazamo yao na kukubali kukosolewa kwa misingi ya kuboresha.

Ralf Rangnick

Hili linapewa nguvu na Ralf Rangnick ambaye kwa upande wake, anapokea wazo hili na kufungua milango kwa wachezaji kusemezana wenyewe kwa wenyewe, ndani na nje ya vyumba vya kubadilishia nguo.

Ralf Rangnick anasema;

Tunapaswa kufanya kazi na kuwa bora wote kwa pamoja kama timu. Kama ni muhimu kuzungumza na wachezaji moja kwa moja kwenye vyumba vya kubadilishia nguo, itasaidia.

Kwa mfano, kama Cristiano au mchezaji mwingine yeyote akifanya hivyo kwa wachezaji wenzake ndani na nje ya uwanja, ninawakaribisha kufanya hivyo.

Njia pekee ya kuboresha na kukuza wachezaji, ni kuboresha kiwango cha timu kwa pamoja.

Man United watakua uwanjani wikiendi hii kupambana na Aston Villa katika muendelezo wa EPL. Bofya hapa, kutandaza jamvi lako na Meridianbet.


JIACHIE NA ALMIGHTY AZTEC

Ni muda wako kujiachia na mchezo maridhawa wa Almighty Aztec katika kasino bomba za meridianbettz. Nafasi ya kutengeneza mkwanja iko mikononi mwako kazi ni kwako.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe