Nahodha wa Real Madrid, Sergio Ramos ameripotiwa kuwa katika hatihati ya kusaini mkataba mpya wa mwaka mmoja huko Bernabeu.

Mkataba uliopo wa beki huyo wa kati na Los Blancos unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa mwezi Juni, ikimaanisha kwamba, kama ilivyo, ataondoka klabuni kwa uhamisho wa bure katika wiki zijazo.

Ramos alidhaniwa kuwa alikuwa akisikiliza nia ya mkataba wa muda mrefu badala ya dili la mwaka mmoja liliowekwa mezani na miamba ya La Liga.

Sergio Ramos madrid

Lakini kwa mujibu wa Deportes Cuatro, kijana huyo wa miaka 35 amefanya U-turn na sasa yuko tayari kupokea mkataba mpya huko Bernabeu hadi Juni 2022.

Kocha mpya wa Real Madrid Carlo Ancelotti hivi karibuni alisema kuwa alikuwa na nia ya kumbakiza “mchezaji muhimu sana” Ramos klabuni hapo kuelekea msimu ujao.

Staa huyo wa zamani wa Sevilla, ambaye kwa utata aliachwa kwenye kikosi cha Uhispania cha Euro 2020, alifunga mara nne na kusajili asisti moja katika mechi 21 kwenye kiwango cha kilabu msimu uliopita.


WEKA PESA KUPITIA DUKANI MERIDIANBET!

Chukua namba yako ya akaunti na kiasi cha pesa unachotaka kuweka, sogea kwenye duka lolote la Meridianbet lililo karibu nawe utasaidiwa kuweka pesa.

Weka Pesa Meridianbet

WEKA PESA

4 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa