Sean Dyche Atoaneno Mkataba wa Tarkowski

Kocha wa Burnley – Sean Dyche amesisitiza “hana tatizo” na beki wake Tarkowski. Hii ni baada ya mchezaji huyo kusema hadharani hana mpango wa kusaini mkataba mpya.

Wiki iliyopita, Tarkowski aliweka hadharani adhma yake ya kutohitaji kusaini mkataba mpya wa kuendelea kubaki Turf Moor. Jambo hili limezua taharuki miongoni mwa mashabiki wa Burnley ikizingatiwa kwamba usajili uliopita, timu hiyo iligoma kumuachia kwa pauni 30 zilizotolewa na Leicester City.

Licha ya kucheza michezo 6 msimu huu, Tarkoswski alinukuliwa akisema “Hakuna nilichokisikia au kupatiwa ambacho pengine kitanifanya nifikirie kusaini mkataba mpya na Burnley

Tarkowski
James Tarkowski.

Akijibu tamko hilo, Sean Dyche amesema “siku hizi wachezaji wanauwazi wa aina yake kwenye media na kulingana na maswali tofautitofauti. Aliulizwa maswali na aliyajibu kwa ukweli kama ilivyoonekana.

“Haya mambo yanatokeaga muda mwingi, sina tatizo na Tarky au mtu yeyote, ni mchezo mzuri sana kwetu, kwangu ni mchezaji mwenye kiwango kikubwa.

“Nimelisema hili kwa mwezi mzima sasa… ninashangaa kwanini hausishwi kwenye timu ya Taifa ya Uingereza, ninadhani anapaswa kupewa hiyo nafasi.

“Yale mahojiano hayabadilishi kitu chochote, zaidi anapaswa kuongeza juhudi na kufanya vizuri kwenye uchezaji wake, kwenye timu na klabu kwa ujumla. Sidhani kama hilo litabadilisha kitu chochote.”

Je, Sean Dyche atafanikiwa kumbakiza Tarkowski kwenye kikosi cha Burnley au beki huyo ataendeleza msimamo wake? Leicester City na West Ham United ni miongoni mwa timu zilizokuwa zinawania saini ya mchezaji huyo kwenye dirisha la usajili lililopita.


BASHIRI UKIWA MAHALI POPOTE!

Hauhitaji kuwaza linapokuja suala la ubashiri na odds kubwa. Bashiri na Meridianbet ukiwa popote ufurahie ushindi mkubwa katika michezo mbalimbali na hadi milioni 16 kwenye michezo ya kasino.

Meridianbet Beti Popote

INGIA MCHEZONI!

23 Komentara

    Duu mbona hiyo shida kugoma kusain mkataba mwingine ngoja tuone

    Jibu

    Tunasubiri tuone

    Jibu

    Dhuuu hayo mapyaa

    Jibu

    Dash Mimi naona kama kunamkanganyiko hapo mana kila mtu anajambo lake nafikiri waelewane vizuri kuhusu mkataba mambo mengine yaendelee

    Jibu

    Sawa tu.ashikilie msimamo wake

    Jibu

    Du! Ana msimamo mkali!!!

    Jibu

    Tunasubiri kwa hamu

    Jibu

    kama kaamua kutokuongeza mkataba wasimlazimishe wampe muda wa kuchagua nini anataka

    Jibu

    Inabid wakae chin waelewan waje na jibu moja

    Jibu

    vzr

    Jibu

    Tuna subili

    Jibu

    Safi

    Jibu

    Tunasubilia tuone

    Jibu

    Fresh

    Jibu

    Nice information

    Jibu

    Basi sawa

    Jibu

    Safi

    Jibu

    Tarkowiski hinatakiwa hakacheze vilabu vikubwa ili kuliendeleza soka lake

    Jibu

    Imeisha iyoooo

    Jibu

    Safii

    Jibu

    Nice

    Jibu

    Safi

    Jibu

    Hataki kubaki sehemu moja

    Jibu

Acha ujumbe