Tetesi zinasema Chelsea tayari inafanya mazungumzo na mlinzi wa Brazil Thiago Silva, 36, kuhusu kuongezwa kwa kandarasi yake kwa mwaka mwingine hadi 2022.

Arsenal inamfuatilia aliyekuwa mchezaji wao Yunus Musah, 17, huku Everton, Leeds na Wolves zikiwa zimeonesha nia ya kutaka kumsajili winga huyo wa Valencia, ambaye pia ni mchezaji wa kimataifa Marekani.

Ajax ina nia ya kumsajili beki wa kushoto wa Crystal Palace na Uholanzi Patrick van Aanholt, 30, katika makubaliano ya kabla ya mkataba Januari.

 

Tetesi za Soka Barani Ulaya.

Real Madrid imejibu tetesi za Raphael Varane kuhusishwa na Manchester United kwa kusema mlinzi huyo wa Ufaransa, 27, “hawezi kuuzwa”.

Arsenal iko tayari kufanya mazungumzo na Nicolas Pepe baada ya kupewa kadi nyekundu huko Leeds Jumapili lakini hakuna uwezekano wa kufikiwa kwa makubaliano ya mkopo dhidi ya mshambuliaji huyo wa Ivory Coast forward, 25, Januari.

Legendi wa Soka Diego Armando Maradona Amefariki dunia Jioni ya jana baada ya kupata shambulio la moyo siku chache tangu aliporuhusiwa kutoka hospitali, alikofanyiwa operesheni ya kuondoa damu iliyoganda kwenye ubongo.

Tetesi zinasema Bayern Munich imeamua kutotoa ofa kwa Jerome Boateng, 32, ya mkataba mpya wakati mkataba wa mlinzi huyo wa Ujerumani unakamilika msimu ujao.

Inter Milan inataka kuwa na uhakika wa kuwa na mkataba mpya na Lautaro Martinez, 23, kabla ya dirisha la usajili kufunguliwa Januari baada ya mshambuliaji huyo wa Argentina kuanza kunyatiwa na Barcelona.

 

Tetesi za Soka Barani Ulaya.

Kiungo wa kati wa Croatia Luka Modric, 35, ana hamu kubwa ya kuendelea kusalia Real Madrid hata baada ya kumalizika kwa mkataba wake msimu ujao.

Mchezaji wa Real Madrid Isco, 28, anataka kuondoka La Liga. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uhispania awali amehusishwa na Ligi ya Premier.

Tetesi zinasema kiungo wa kati wa Uturuki Yusuf Yazici, 23, anatarajiwa kuongezewa mshahara wake kutoka Lille baada ya Arsenal kuonesha nia ya kutaka kumsajili.

Tetesi zinasema aliyekuwa mchezaji wa Inter Milan, Manchester City na Brazil beki wa kulia Maicon, anafanya mazungumzo ya kujiunga na Ligi ya Italia ya Serie D, Sona.

Mshambuliaji aliye kwa mkopo katika klabu ya Getafe, Hugo Duro, 21, huenda akajiunga na Real Madrid Jumatano, usiku wa kabla ya mwanafunzi huyo wa Uhispania kufanya mtihani wake wa uhandisi katika masomo ya kiufundi.

Aliyekuwa mshambuliaji wa Manchester City, Manchester United na West Ham Carlos Tevez, 36, yuko tayari kustaafu Boca Juniors na Argentina na anatarajiwa kujiunga na siasa.

Tetesi zinasema aliyekuwa rais wa Barcelona Joan Laporta yuko tayari kujitangaza kama mgombea katika uchaguzi wa urais ujao katika klabu hiyo ya Uhispania.


USICHELEWE KUKAMATA MKWANJA HUU!

Hadi 130,000,000 TSH Kutolewa kwa washiriki wa shindano la Playson Cashfall. Unaipata kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet Pekee. Jisajili sasa, kisha ingia mchezoni kabla ya Novemba 29.

Meridianbet Tanzania Casino

SOMA ZAIDI

18 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa