Tetesi zinasema, Mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, 22, amekataa ofa ya kuongeza mkataba na Paris St-Germain, ambao unamalizika msimu ujao na badala yake angependelea kujiunga na Real Madrid msimu huu.
Beki wa kati wa Uhispania Pau Torres, 24, amekataa kuhamia Tottenham Hotspur kwasababu haiwezi kushiriki Ligi ya Champions msimu huu ilihali klabu yake ya nyumbani Villarreal.
Tetesi zinasema, Maxwel Cornet, 24, anakaribia kuelekea Burnley, ambayo ofa yake ya karibu pauni milioni 12 na marupurupu mengine ikiwa yameshinda dau kutoka Hertha Berlin.

Tetesi zinasema, Leeds United inataka kumpatia mshambuliaji wa Uingereza Patrick Bamford, 27, mkataba wa muda mrefu kutokana na kuwindwa Tottenham.
Juventus inataka kumsajili tena Miralem Pjanic, 31, mwaka mmoja baada ya kumuuza kwa Barcelona, mabingwa hao wa Uhispania wako tayari kumuachia kiungo huyo wa kati wa Bosnia kuondoka bila malipo.
Tetesi zinasema, Chelsea, Manchester United na Manchester City zote hizo zina mnyatia kiungo wa kati wa Metz raia wa Senegal Pape Matar Sarr, 18.
Tetesi zinasema, Fiorentina imekataa dau la Atletico Madrid la euro milioni 60 sawa na (£51m) kwa ajili ya mshambuliaji wa Serbia Dusan Vlahovic, 21, ambaye pia ana nyatiwa na Tottenham.

Atletico Madrid sasa imeonesha nia ya kumsajili mshambuliaji wa Brazil Matheus Cunha, 22, kutoka Hertha Berlin huku mazungumzo ya kumsajili mshambuliaji wa Uhispania Rafa Mir, 24, kutoka Wolves yakiwa yamekwama.
West Ham United ilipoteza dhidi ya Roma katika kinyanganyiro cha kumsajili mshambuliaji wa England Tammy Abraham kutoka Chelsea baada ya kushindwa kutimiza matakwa ya mshahara wa mchezaji huyo, 23.
Baada ya kuondoka Crystal Palace msimu huu, Gary Cahill anahitajika katika uhamisho wa bure na Bournemouth huku Norwich City na Rangers pia nazo zikionesha nia ya kumsajili mchezaji huyo aliyekuwa mlinzi wa England, 35.
Ni muda wa kuwa milionea na kasino za mtandaoni za meridianbet, mchezo wa Sahara Riches unakupa nafasi ya kushinda mkwanja mrefu. Matajiri wa jangwani wanataka wakupe mkwanja leo.


