Tetesi zinasema, Maafisa wa Barcelona wamefanya mazungumzo na Manchester City kuhusu kumsajili mshambuliaji wa Uhispania Ferran Torres, 21, mwezi Januari.
Tetesi zinasema, Manchester City wanamfuatilia mshambuliaji wa Fiorentina na Serbia Dusan Vlahovic. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 amefungia mabao 19 klabu na taifa msimu huu.

Tetesi zinasema, Mwenyekiti wa Everton Bill Kenwright ameitisha kikao cha dharura cha bodi, huku mustakabali wa kocha Rafael Benitez ukitarajiwa kujadiliwa.
Everton wanafikiria kumnunua mshambuliaji wa Zenit St Petersburg na Iran Sardar Azmoun, 26, ambaye hapo awali amekuwa akihusishwa na West Ham, Tottenham na Arsenal.
Kiungo wa kati wa Inter Milan na Denmark Christian Eriksen, 29, anakaribia kukatiza kandarasi yake. Eriksen hajacheza tangu alipopatwa na mshtuko wa moyo kwenye Euro 2020.
Tetesi zinasema, Real Madrid wana uhakika kuwa watamsajili mshambuliaji wa Paris St-Germain Mfaransa Kylian Mbappe, 22, ambaye kandarasi yake itakamilika msimu ujao.

Manchester United wanaweza kumuomba kocha wa Austria wa New York Red Bulls Gerhard Struber kuwa msaidizi wa Ralf Rangnick. Wawili hao walifanya kazi pamoja katika klabu ya Red Bull Salzburg.
Tetesi zinasema, Kiungo wa kati wa Barcelona na Uholanzi Frenkie de Jong, 24, hataondoka mwezi Januari. De Jong amekuwa akihusishwa na klabu kadhaa ikiwemo Manchester City.
Mkufunzi wa Newcastle, Eddie Howe anasema mshambuliaji wa Kiingereza Dwight Gayle, 32, yuko kwenye mipango yake baada ya mchezaji huyo kuhusishwa na kurejea katika klabu ya West Brom, ambapo alifunga mabao 24 alipocheza kwa mkopo msimu wa mwaka 2018-19.
Mabingwa Meridianbet hawajawahi kukuacha mnyonge hasa katika kipindi hiki cha msimu wa sikukuu, kasino maridhawa ya Carnaval Jackpot inakupa thamani ya dau lako. Kuwa mmoja wa washindi leo hii.


