Ronaldo Vilabu vya Uingereza na Amerika ni Ghali Sana

Mshambuliaji wa zamani wa taifa la Brazil Ronaldo De Lima alisema kuwa kabla ya kwenda Hispania kununua klabu ya Real Valladolid, alitaka kununua klabu kwenye ligi ya Uingereza Championship na MLS ya Marekani.

Ronaldo ametumia karibia miaka 20 kwenye soka kama mchezaji, huku akipita kwenye vIlabu kadhaa vikubwa kwenye bara la Ulaya kama Real Madrid, Barcelona, Juventus, Inter Milan, Ac Milan na vingine vingi, lakini pia amefanya makubwa akiwa na timu yake ya taifa ya Brazili huku akichukua kombe la Dunia mara mbili na kushinda kiatu cha dhabu 2002.

mwaka 2011 alionyesha nia ya kutaka kununua timu ya mpira wa miguu na kwa mara ya kwanza aivutiwa na kununua timu ya ligi kuu marekani MLS kabla ya kuamua kwenda europe nchini uingereza kwenye ligi ya Championship.

“Nilikwenda jijini New York na kufanya kikao na raisi wa ligi ya MLS na aliwasilisha mawazo yake, unaweza shinda kila kitu unachotaka, kama huna  €70milioni, unaweza kwenda sehemu nyingine.” Ronaldo De Lima

“Pia ikabidi nihamie ulaya kwenye ligi ya championship nchini uingereza, lakini kila kitu kilikuwa ghalama pasipo kuwa na £60milioni huwezi pata timu, ikabidi niangalie sehemu nyingine kama Ureno na Hispania kwenye unafuu na kufanikiwa kupata nafasi Real Valladolid.” Aliongezea  Ronaldo

Ronaldo amenunua hisa asilimia 51 kwenye klabu ya Real Valladolid miaka mitatu iliyopita na tangia hapo, amekuwa raisi wa timu hiyo mpaka sasa.


MUDA WA KUJIACHIA NA CARNAVAL JACKPOT

Mabingwa Meridianbet hawajawahi kukuacha mnyonge hasa katika kipindi hiki cha msimu wa sikukuu, kasino maridhawa ya Carnaval Jackpot inakupa thamani ya dau lako. Kuwa mmoja wa washindi leo hii.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.