Tetesi zinasema, Arsenal wamefanya mazungumzo kuhusu uhamisho wa mshambuliaji wa Napoli na timu ya taifa ya Nigeria Victor Osimhen, 23, na wanaendelea na jaribio la kumnyakua mshambuliaji Gabriel Jesus, 25, kutoka Manchester City.
Mshambuliaji wa Uruguay Luis Suarez, 35, huenda akahamia klabu ya Inter Miami ya David Beckham inayoshiriki ligi ya Major League baada ya kuachiliwa na Atletico Madrid.
Tetesi zinasema, Kocha mkuu wa Chelsea Thomas Tuchel anatazamiwa kuwa na pauni milioni 200 za kutumia msimu huu wa joto huku baada ya Todd Boehly kukubaliwa kumiliki timu hiyo.
Winga wa Brazil Raphinha, 25, amewaambia wakurugenzi wa Leeds United kwamba anataka kuchezea Barcelona, ambao walitoa dau la £30m lililokataliwa mapema mwezi huu.
Mshambuliaji wa Ubelgiji Eden Hazard, 31, hana mpango wa kuondoka Real Madrid, amesisitiza kuwa anataka sana kuonyesha uwezo wake baada ya miaka mitatu yake Real kugubikwa na majeraha.
Tetesi zinasema, Everton na Crystal Palace wanataka kumsajili winga wa Watford na Senegal Ismaila Sarr, lakini Newcastle wamestitisha azma yao ya kumsaka kiungo huyo wa miaka 24.
Mlinzi wa Sevilla na Ufaransa Jules Kounde, 23, na Croatia na kiungo wa kati wa RB Leipzig Josko Gvardiol, 20, wako kwenye orodha ya wachezaji wanane wanaotarajiwa kusajiliwa na Chelsea msimu wa joto.
Tetesi zinasema, Mlinzi wa Arsenal na Ufaransa William Saliba, 21, atakuwa sehemu ya kikosi cha Gunners ch amsimu ujao baada ya kuvutia wakati wa mkopo huko Marseille.
Aston Villa wameungana na Everton katika mbio za kutaka kumsajili kiungo wa kati wa Burnley James Tarkowski, 29, huku beki huyo akipatikana kwa uhamisho wa bure.
West Ham wanaendelea kufanya mazungumzo na klabu ya Rennes kuhusu mkataba wa mlinzi wa kati wa Morocco Nayef Aguerd, 26, na wanakaribia kuafikiana kuhusu bei yake.
Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.