Tetesi zinasema Liverpool wamemfuatilia Ismaila Sarr na kujadili suala lake na Watford, ambayo inataka pauni milioni 36 kwa ajili ya mshambuliaji huyo.
Sarr pia anawindwa na Manchester United kama mbadala ikiwa mpango wa kumnasa winga wa Borussia Dortmund Jadon Sancho utashindwa.
Mashetani wekundu pia wanafikiria uhamisho wa winga wa Inter Milan Ivan Perisic, 31, Kingsley Coman,24 anayekipiga Bayern Munich na Douglas Costa kutoka Juventus.

Manchester United wanamfuatilia kiungo wa kati wa Ujerumani Sami Khedira,33, mkataba wake na Juventus utakapokwisha.
Wakala wa Edouard Mendy amedai kuwa makubaliano yameafikiwa kwa ajili ya mlinda mlango huyo, 28, anayekipiga katika klabu ya Rennes kujiunga na Chelsea.
Brentford amekataa ofa ya takriban pauni milioni 10 kutoka Arsenal kwa ajili ya mlinda mlango David Raya, 25.
Tetesi zainasema Southampton imeaiambia Tottenham kuwa mshambuliaji Danny Ings,28, hauzwi kwa dau lolote.
Leicester City iko karibu kumsajili kwa mkopo mshambuliaji wa Uturuki Cengiz Under,23, kutoka Roma na mlinzi wa Burnley James Tarkowski,27, bado anatolewa macho na Brendan Rodgers.

West Ham imebadili muundo wa ofa kwa ajili ya kumnasa Tarkowski lakini ofa hiyo bado imekataliwa na Burnley.
Tetesi zinasema West Brom wanajaribu kumsajili mshambuliaji wa Aston Villa, Mbwana Samatta, kabla ya mchezaji huyo mwenye miaka 27, hajamaliza mchakato wa kuhamia Fenerbahce.
Mlinzi wa zamani wa Liverpool Nathaniel Clyne anafanya mazoezi na klabu ya Crystal Palace na anaweza kupata mkataba na klabu hiyo ya Selhurst Park .
Edin Dzeko anajiandaa kujiunga na Juventus akitokea Roma kwa mkataba wa miaka miwili. Uhamisho wa mshambuliaji wa Herzegovina,34, utamaanisha kuwa matumaini ya Luis Suarez kutoka Barcelona huenda yakafikia mwisho.

Tetesi zinasema Arsenal wamekubali masharti ya kiungo wa kati wa Lyon Houssem Aouar, 22.
Kiungo wa kati wa Tottenhan Dele Alli,24, ameibuka kuwa mlengwa wa Paris St-Germain na Inter Milan.
Tetesi zinasema Mshambuliaji wa Serbia Luka Jovic,22, anafikiria kuondoka Real Madrid.
Genoa wamefikia makubaliano na Chelsea kumsajili kwa mkopo beki wa kulia wa Chelsea Davide Zappacosta, 28.
SHINDA NA MERIDIANBET!
Tengeneza pesa kidijitali kwa kubashiri mbio za farasi hapa Meridianbet! Chagua nani ashinde, unakusanya mkwanja.


Shani
Asnte kwa Makala yenye habar moto moto!!
Rose kapinga
Mambo ya mkwanja yanahusika hapo!!
Povel
Nice update
magdalena
liverpool wamuachie tu uyo sarri ili atue united
Genia Sikaluzwe
Ahsant sana meridianbet kwa taarifa
Nasra
Gud
Lydia Emmanuel Magoti
Mambo mazuri na pesa nje nje
Dorophina
Sancho akienda man u itakuwa poa kinyama
Mwanahamisi
Mambo ya mkwanja nje nje
Njiku
Man u bhana sijui wanabugi wapi naona wanahitaji wazee sasa ili timu ifanye poa imekuwa club za Italy dah
Sauda
Sancho akitua Liverpool atakuwa ameula
Fatina
Mambo Ni mazuri
Caroline
Asante kwa taarifa
Zeiyana
Chelsea ya sasa si ya mchezo mchezo tumeona imesajiri wa chezaji wengi mwenye uwezo na kipa pia hii ni habari njema kwa mashabiki wa Chelsea
Tatu
Usajili naona umezidi kupamba moto
Mwajumah
Asante kwa makala#Meridianbettz
Ernest
Kweli Juventus ni Kibibi kizee
Saupha mohamed
Asanteni kwa taarifa
Khadija
Habari njema#meridianbettz
Latifa juma mohamed
Gud
Gabriel
Imekaa poa sana 👍
Hopemwaikuka
🙌
Janeflora malisa
Nice
Issa
United hawafany wanaongea tu
Sabrina
Usajili umepamba moto
Salma ngende
Imekaa poa
Samiah
Imetulia hiyo
Angelina
Goodupdate
Amiri Kayera
Habar Nzur za usajir
felister
usajili unazidi pamba moto