Kagere ni Mzuri ila Bocco ni Bora

Kocha wa Simba Sven Vandenbroeck anayahusudu sana matumizi ya mshambuliaji mmoja kuliko wawili. Na hii ndiyo sababu inayomuweka Meddie Kagere benchi. Haijawa rahisi kwa Kagere kufua dafu mbele ya John Bocco tangu mwisho wa msimu uliopita. Sven anaona mbinu zake zikifanya kazi zaidi ndani ya Bocco kuliko Kagere. Ndiyo maana hampi nafasi Meddie Kagere katika kikosi cha kwanza. Subiri kwanza, huyu ndiyo mfungaji bora wa ligi kwa misimu miwili iliyopita.

Tofauti na kufunga, Bocco ni mzuri wa kutunza mipira na kutengeneza nafasi. Mikimbio ya Bocco inawaruhusu viungo kuingia kwenye box na kufunga. Hivo ukiwa na Bocco uwanjani, unakuwa na hakika ya kupata mabao kutoka maeneo mengi ya uwanja. Kagere ni mfungaji zaidi. Anahitaji kupikiwa zaidi ili upate mabao ila yeye si mpishi wala si mtengenezaji sana. Nadhani ni hii sababu inayompa Bocco nafasi zaidi ya Kagere.

Nilimsikia shabiki mmoja akilalamika kwamba, kwanini kocha hawachezi wote wawili? Sawa wanaweza kucheza wote wawili, ila tumewaza nani atampisha Kagere ili waanze pamoja na Boccco. Ili Kagere na Bocco waanze kwa pamoja, ina maana kati ya Chama, Morrison na Miquissone mmoja lazima akae benchi. Tupo tayari kumuona mmoja kati ya hao akikaa benchi? Usinijibu.

Nilimsikia mwingine akisema, kwanini Simba imesajili washambuliaji wengine wapya kama kocha anamtumia mmoja tu. Nadhani alikuwa anahusisha ujio wa Chris Mugalu na Charles Ihafya. Ila hii ndiyo maana ya kikosi kipana. Tusisahau kuwa Ferguson aliwahi kuwa na Ole Gunner Solksjaer, Teddy Sheringham, Andy Cole na Dwight Yorke kwenye timu moja. Tusisahau!

Kwa maoni yangu mimi, nadhani Sven hakosei kuanza na mshambuliaji mmoja, nadhani hakosei kuwa na Bocco kama namba moja wake, nadhani pia Simba haikukosea kuleta washambuliaji wengine wapya.


SHINDA NA MERIDIANBET!

Tengeneza pesa kidijitali kwa kubashiri mbio za farasi hapa Meridianbet! Chagua nani ashinde, unakusanya mkwanja.

Cheza Sasa.

28 Komentara

    Mashabiki tunashukuru kusikia hivyo@meridianbettz

    Jibu

    Kegere ni mzuri sana!!

    Jibu

    Kagere fundi

    Jibu

    Kocha falsa zake zinamshusha kiwango cha mkali wa kucheka na nyavu mamba meddier kagere ni kwl kagere Bora kwa nyavu bocco ni machepele

    Jibu

    pamoja ya kuwa kagere ni fundi wa mpira ila bocco naye ni noma aswa akiushika mpira hakubali kuuachia kirahisi

    Jibu

    Kagere jembe

    Jibu

    Kagere jembe

    Jibu

    Mmeshamtumia kagere wa watu mmemchoka mnaamua kumuweka benchi mwisho wa siku mtamuuza

    Jibu

    Kagere kiongozi

    Jibu

    Wote wanahunuhimu kwa klabu yao kwangu wote bora

    Jibu

    Mm naona wote bora maan awawezi kulingan Kila mmoja anaujuzi wake!!

    Jibu

    Wote wapo vizuri

    Jibu

    Kagere hana maajabu yoyote sikuizi na ndio maana uwongozi wa simba wamesajili washambuliaji wengi hatatumiwa kwa ziada tu na sio kutolewa macho kama zamani

    Jibu

    Wote wazuri wanategemeana na msimu naona sasa kagere hana chake pale simba

    Jibu

    Kagere ndio chombo bhana#Meridianbettz

    Jibu

    Napata kigugumizi kidogo kama mdau wa Soka lakini mwisho wa siku kutokana na usajili ulivyofanywa na Simba basi Double striker itahusika suji nani atakaa benchi wakati hili linatokea lakini ndio njia pekee, Mmoja wa kutupia sana magoli na mwingine kutengeneza nafasi ni kuwa na uhakika wa kushinda mechi 100% hapo bado usajili mpya ambao wao ni backup.

    Jibu

    Kegere mi naona ni bora zaidi

    Jibu

    Kagera MTU mbayaaa

    Jibu

    kagere namkubali#meridianbettz

    Jibu

    Bocco ni mzuri wa kutunza mipira na kutengeneza nafasi. Mikimbio ya Bocco inawaruhusu viungo kuingia kwenye box na kufunga. Hivo ukiwa na Bocco uwanjani, unakuwa na hakika ya kupata mabao kutoka maeneo mengi ya uwanja. Kagere ni mfungaji zaidi. Anahitaji kupikiwa zaidi ili upate mabao ila yeye si mpishi wala si mtengenezaji sana. Nadhani ni hii sababu inayompa Bocco nafasi zaidi ya Kagere.

    Jibu

    Wapo vzr wote

    Jibu

    Bocco ni kifaa sana

    Jibu

    Fundi wao

    Jibu

    Mila mchezaji ana ubora wake

    Jibu

    Kwer kabisa Bocco ni bora

    Jibu

    Bocco yuko vizuri

    Jibu

    Tumuachie coach kaz yake

    Jibu

    kila mmoja ana ujuzi wake

    Jibu

Acha ujumbe