Juan Bernant huenda akakosa michezo kadhaa msimu mpya 2020-21 baada ya Paris Saint-Germain kuthibitisha beki huyo kusumbuliwa na jeraha la goti.
Bernat alitolewa nje baada ya kuumiza goti lake katika dakika za mwisho kwenye mchezo dhidi ya Metz Siku ya Jumatano na kupata ushindi mwembamba wa 1-0.
Beki huyo wa zamani Bayern Munich alitolewa dakika ya 86 na aliingia dakika 63 kabla ya Julian Draxler hajatikisa nyavu za Metz na kuifanya PSG ipate ushindi wa kwanza kwa msimu 2020-21.

Sasa PSG wameeleza kwamba Bernat atakaa nje ya dimba huku akaiendelea kujitizamia kutokana na jeraha lake la ACL na taarifa zaidi zitatolewa siku zijazo.
Wakati kukiwa hakuna taarifa rasmi ni lini Bernat atarejea lakini taarifa za awali zinadai Bernat atakaa nje kwa kipindi kisichopungua miezi sita.
Kuumia kwa Bernat itakuwa ni pigo jingine kwa PSG baada ya wachezaji watatu wa PSG kupata adhabu ya kuikosa michezo kadhaa baada ya kuoneshwa kadi nyekundu katika mchezo dhidi ya Maraseille, wachezaji hao ni Neymar,Leandro Paredes na Kurzawa lakini Mbappe anatumainiwa kurejea baada ya kutoonesha dalili za COVID-19.
Mauro Icardi na Marquinho walicheza dakika 90 baada ya kurejea kutoka karantini na watacheza dhidi ya Nice siku ya Jumapili.
SHINDA NA MERIDIANBET!
Tengeneza pesa kidijitali kwa kubashiri mbio za farasi hapa Meridianbet! Chagua nani ashinde, unakusanya mkwanja.


Aziza mushi
Asanten kwa habari
Povel
Get well soon 🙏🏼🙏🏼🙏🏼#Bernat
Zeiyana
Wana ali ngumu sana PSG kwa staili sijui kama wataweza kufunzu ligi ufarasa
Shani
Mungu amtie nguvu
Adelta
PSG wanahali ngumu kwa sasa @meridianbettz
magdalena
duh aya kweli ni majanga PSG wana mapengo mengi sana juu ya wachezaji
Tatu
Psg kunani mbona wameaza na msimu mbaya kuasi hichi
Ernest
Huu ni mzimu wa kushindwa kuchukua UEFA wakati walikuwa na sababu zote kuweza kushinda, tusipoangalia PSG watapotelea mbali
Samira
PSG wasipojiangalia watapotelea mbali mapema
Issa
Psg mwaka wao
Salma ngende
Pole yao
Angelina
Get well soon
Amiri Kayera
Msim huu psg wanakaz kubw kueka saw kikos chao
felister
kwa staili hii sijui Kama psg wataweza fuzu