Haijulikani hasa kuna nini kinaendelea kati ya Thomas Tuchel na Romelu Lukaku kule Stamford Bridge. Kuna moshi unafuka, chanzo cha moto ni nini?
Lukaku alifanya mahojiano na kituo cha Sky Sport wiki iliyopita. Miongoni mwa mengi aliyozungumza, mshambuliaji huyo alisema hadharani kuwa hafurahii maisha ndani ya Chelsea na kwamba, Tuchel ameamua kutumia mfumo ambao ni tofauti na alivyoaihidiwa wakati anasajiliwa.
Lukaku amekuwa akisugua benchi kwa muda sasa tangu alipopata majeruhi. Nafasi yake kwenye kikosi cha Chelsea haijulikani kwa sasa. Ni mfumo wa kocha au uwezo wa mchezaji ndio changamoto.
Kufuatia mahojiano yake na Sky Sport ambayo pia yamezua gumzo kwenye vyombo vya habari, Thomas Tuchel aliamua kumuacha Lukaku kwenye orodha ya wachezaji watakaohusika kwenye mchezo dhidi ya Liverpool wikiendi iliyopita.

Baada ya kutoka sare ya 2-2 dhidi ya The Reds, kocha huyo ameweka wazi kuwa atafanya mazungumzo ya ana kwa ana na Lukaku. Lengo likiwa ni kujua tatizo lake ni nini na maamuzi yatafanyika baada ya mazungumzo hayo.
Mpaka sasa, ni mpambano wa Thomas vs Lukaku, Chelsea kama klabu haijatoa tamko lolote na inadaiwa kuwa, uongozi wa timu hiyo unasubiri maamuzi ya kocha. Pia, The Blues hawana mpango wowote wa kuachana na Lukaku kwenye majira haya ya baridi.
Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.


