Tetesi zinasema, Mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku, 28, hana furaha kuwa Chelsea na huenda akajaribu kuungana na kocha wake wa zamani Antonio Conte katika klabu ya Tottenham msimu wa joto.
Tetesi zinasema, Barcelona huenda wakamruhusu winga wa Ufaransa Ousmane Dembele, 24 kujiunga na Manchester United ili kuweza kuipata saini ya Anthony Martial, 26.
Manchester United wana matumaini ya kumsajili kiungo wa kati wa Ungereza Declan Rice, 22 kutoka West Ham wakati Manchester City na Chelsea wamekuwa wakivutiwa na mchezaji huyo kwa muda mrefu.

Newcastle wanataka kuwasajili wachezaji sita dirisha la usajili litakapofunguliwa mwezi huu wa Januari na wana matumaini ya kumpata beki wa kulia wa Atletico Madrid na Uingereza Kieran Trippier, 31.
Tetesi zinasema, Tottenham na West Ham ni miongoni mwa klabu zinazomtaka mshambuliaji wa Uhispania Adama Traore, 25, Wolves wako tayari muuza kwa pauni milioni 20 kufadhili bajeti yao ya uhamisho.
Meneja wa Real Madrid Carlo Ancelotti amependekeza klabu hiyo ya Uhispania itasubiri hadi msimu wa joto kufanya harakati za kumsajili mshambuliaji wa Paris St-Germain Kylian Mbappe, 23.

Tetesi zinasema, Liverpool na AC Milan wanataka kumsajili kiungo wa kati wa Guinea Aguibou Camara, 20, kutoka klabu ya Ugiriki ya Olympiakos.
Aston Villa ndio klabu ya hivi punde zaidi ya Ligi ya Premia kuhusishwa na kiungo wa kati wa Borussia Monchengladbach ya Uswizi Denis Zakaria, 22 mchezaji huyo ananyatiwa na Liverpool, Leicester City, Arsenal na Everton.
Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.


