Uchambuzi Mchezo wa Sheffield United Dhidi ya Chelsea.

Huku Ratiba ya EPL ikionyesha zimebaki mechi 4 tu msimu kumalizika, Chelsea hadi sasa wamekaa nafasi ya 3 alama mbili tu mbele ya Manchester United iliyopo nafasi ya tano, pambano la leo dhidi ya timu ya Chris Wilder wa Sheffield ni shoo nyingine nzito kwa Blues kwani lazima kushinda kujihakikishia nafasi kwenye Ligi ya Mabingwa msimu ujao .

Ugumu wa game ya leo ni kwamba Sheffield United pia wanatamani kucheza mashindano ya Ulaya msimu ujao, hii haitakuwa mechi rahisi na inaweza kushinda timu yoyote.

The Blade – Timu ya Sheffield United

Chini ya kocha wake mahili Chris Wilder, Sheffield wamekuwa na maajabu msimu huu. Licha ya bajeti ndogo, timu inakimbikiza katika Ligi, na sasa wamekaa katika nafasi ya saba kwa alama 51, mbele ya wakongwe kama Arsenal na Spurs.

Kwa kuzingatia kwamba ni timu mpya iliyopanda daraja msimu huu. Kuingia kwenye mchezo dhidi ya Chelsea, Blades hawajapoteza katika michezo yao mitano ya nyumbani.

Sababu kubwa ya kufanikiwa kwao msimu huu ni safi yao bora ya ulinzi yenye watu watano ambao wameruhusu mabao 33 tu, na kuifanya kuwa ya nne katika timu zilizoruhusu mabao machache msimu huu pamoja na Manchester United, Liverpool na Leicester City.

Kikosi cha Sheffield United dhidi ya Chelsea.

Golikipa: Henderson;

Eneo la Ulinzi: Basham, Egan, O’Connell;

Eneo la kati: Baldock, Lundstram, Norwood, Berge, Stevens;

Washambuliaji: Sharp, McGoldrick

The Blues – Chelsea

Chelsea inaingia kwenye shoo ngumu dhidi ya vijana wa Wilder, lakini wakiwa katika fomu bora baada ya kushinda mechi nne kati ya tano za Ligi tangu irejee baada ya lockdown.

Kitu kitakachomsumbua kocha mkuu wa timu hiyo, Frank Lampard, ni aina ya wapinzani wawili wanaomfukuza kwa karibu kuwania nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa yani Leicester City na Manchester United, ambao anawazidi alama moja na mbili kwa nyuma.

Kwa hali ilivyo, haitajiki kupoteza katika mechi nne zilizobaki, na Lampard atataka timu yake kuanza kupambana kwenye kila mechi hizo kupata ushindi.

Mahala pekee, panapotia shaka kwa Lampard ni safu yake ya ulinzi ambayo inavuja. Imeruhusu mabao 46 katika mechi 34 za Ligi na wakipata clean sheets mbili tu kwenye mechi 10 za mwisho za ligi.

Kikosi cha Chelsea dhidi ya Sheffield United.

Golikipa: Kepa Arrizabalaga

Safu ya ulinzi: Cesar Azpilicueta, Reece James, Antonio Rudiger, Andreas Christensen, Kurt Zouma, Marcos Alonso, Emerson Palmieri

Safu ya kati: Jorginho, Ruben Loftus-Cheek, Ross Barkley, Mateo Kovacic, Mason Mount

Safu ya ushambuliaji: Willian, Pedro, Christian Pulisic, Callum Hudson-Odoi; Tammy Abraham, Olivier Giroud, Michy Batshuayi, Faustino Anjorin


51 Komentara

    Nice

    Jibu

    Vzur

    Jibu

    Mech itakua nzur

    Jibu

    kwa kikosi hiki nauona ushindi kwa chelsea

    Jibu

    Asante meridianbettz kwa update za michezo#meridianbettz

    Jibu

    sisi wapenzi wa sheffield tunacomment wapi

    Jibu

    Good

    Jibu

    Asante meridianbettz kwa update za michezo#meridianbettz

    Jibu

    Mtanange mgumu sana

    Jibu

    Mechi ngumu sana lakini Chelsea wananafasi kubwa sana ya kunyakuwa point 3 muhimu ukiangalia ubora wa kikosi

    Jibu

    Hii mechi chelsea atafungwa 2-0

    Jibu

    Ushindi kwa chelsea

    Jibu

    Chelsea imeruhusu magoli mengi sana msimu huu. Ina beki line mbovu na hakuna washambuliaji mahiri sana. Ni mechi inayotegemea bahati zaidi#meridianbettz

    Jibu

    Ni meche ngum ila Nampa ushindi Chelsea

    Jibu

    Chelsea afungwe

    Jibu

    Saafi

    Jibu

    Ipo poa hii

    Jibu

    Duuuh! Mchezo utakuwa hatar sana huu

    Jibu

    Mechi kali sana

    Jibu

    Big match iyo

    Jibu

    Safii

    Jibu

    Hii mechi kalii Sana si ya mchezo yaan

    Jibu

    Kivumbi

    Jibu

    Kivyovyote hii ni game ngumu tusishangae chelsea akafa

    Jibu

    Hii mechi ni ngumu kwa kweli

    Jibu

    Mechi ilionekana Kama Chelsea wanashinda lakini gonna likawabadikia

    Jibu

    Mechi kaliiiii

    Jibu

    Sababu kubwa ya kufanikiwa kwao msimu huu ni safi yao bora ya ulinzi yenye watu watano ambao wameruhusu mabao 33 tu, na kuifanya kuwa ya nne katika timu zilizoruhusu mabao machache msimu huu pamoja na Manchester United, Liverpool na Leicester City.

    Jibu

    Mechi itakua poa sana

    Jibu

    Mechi kali#Meridianbettz

    Jibu

    Hii mechi Ni ngumu Ila Chelsea
    Atashinda

    Jibu

    Chelsea nawaona wananafasi kubwa ya kupata point 3

    Jibu

    Majeruhi ni wengi na wanategemewa kwenye timu hivyo Jana palikuwa na upungufu mkubwa hasa upande wa mabeki palikuwa pabovi na kuruhusu magoli hivyo kwa njia hii Chelsea kuwa katika kiwango kinzuri ni bahati nasibu sana haswa kwa mechi ambayo mashabiki wengi wanaisubiria kati ya Chelsea na Manchester united sijui kama wataweza kushinda.

    Jibu

    Safi

    Jibu

    Chelsea kwa nafasi walio kua nayo hinaonesha wamepambana sana hadi kufikia hapo kwa muonekano tu sheffied united hawezi kumfunga chelsea ila kikubwa Chelsea wasijisahau kwani sheffied united pia wanatamani kucheza mashindano ya ulaya msimu hujao

    Jibu

    Kudadeki kivumbi

    Jibu

    Big mechi

    Jibu

    Dakika90 zitaamua#meridianbett

    Jibu

    Chelsea win

    Jibu

    Maoni:safi

    Jibu

    Mechi ngumu sana hii hapo inabidi chelsea ajitahidi haongeze point

    Jibu

    Hii mechi chelsea lazima wafungwe 3-6#meridianbettz

    Jibu

    thankx 4 news

    Jibu

    Uchambuzi unanishawishi kuweka jamvi

    Jibu

    Chelsea ni timu imekuwa ikijitahidi kufanya vizuri Nina Iman ata sasa itafanya vizuri zaidi

    Jibu

    Chelsea kafa

    Jibu

    Mkeka wangu Nampa Chelsea

    Jibu

    ninyi mnawakela watu sasa mtu keshakufa tatu badala ya kumpa pole mnaanza kumwambia umekosea hivi hii sio sawa

    Jibu

    Ilikuwa poa sana#Meridianbettz

    Jibu

    Asante kwa taarifa

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.