United Wamechoma Mikeka Au Newcastle Wametick?

Kwa Man United ya sasa toka ameondoka Ole Gunnar Solksjaer, wadau wengi wa michezo ya kubashiri, wanamuamini. Mwendo wa GG, Over 1.5 zinatoaga, jana vipi?

United walikuwa uwanjani kukabiliana na Newcastle ambayo inahaha kwenye nafasi za kushuka daraja. Manchester waliingia uwanjani zikiwa zimepita siku 16 bila ya kuwa na mchezo kutokana na madhara ya COVID-19 kwenye kikosi hicho.

Mchezo wa kwanza uliochezwa pale Old Trafford, The Red Devils walishinda 4. Bila shaka, huu ulikuwa ni mchezo uliowavuta wachezaji wengi wa michezo ya kubashiri kuweka magoli mengi na pengine kumfuata United moja kwa moja. Mkeka unahali gani?

Mpira ni mchezo wa makosa, Rafael Varane alifanya makosa dakika ya 7 na Allan Saint-Maximin akayatumia makosa hayo na kupachika goli la 1 kwa Newcastle. Umewahi kuwaza, maisha ya Manchester bila David de Gea yangekuwaje?

Golikipa huyu ndio aliwaokoa Manchester kwa sehemu kubwa, mikwaju ya Jonjo Shevley, Migue Almiron, Maximin na ile ya Arthur iliyogonga besela zilikuwa ni nafasi za ushindi kwa Newcastle.

Eeeh bhana eeh!! Utu uzima dawa, Edinson Cavani akitokea benchi kipindi cha pili, anakuja kumuokoa Ralf Rangnick asiambulie kipigo cha kwanza kama kocha wa The Red Devils. Wale wanaouaga timu kubwa, wakaumizwa na Cavani, mkeka huo.. ukaungua.

Kipenga cha mwisho kinalia, ubao wa matokeo unasoma 1-1, umetoboa?


KUWA MILIONEA MSIMU WA SIKUKUU NA SAHARA RICHIES

Unaanzaje siku yako katika msimu huu wa sikukuu, mchongo upo meridianbet kasino. Sloti pendwa ya Sahara Richies inaweza kukufanya ukawa milionea katika kufunga mwaka huu, Jiunge na ufurahie kasino maridhawa kutoka nyumba ya mabingwa.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.