Ralf Rangnick Amjibu Jesse Lingard

Kocha wa muda wa klabu ya Manchester United Ralf Rangnick amekuwa akitoa nafasi kwa wachezaji ili kuweza kumvutia tokea alipochuka mikoba ya kuinoa klabu hiyo huku akitambua kuwa kuna wachezaji wanaotaka kuondoka.

Mmoja wa wachezaji huyo ambaye hajui hatma yake kwenye klabu ya Man Utd ni Jesse Lingard ambaye alimshutumu kwa kuua kipaji chake baada ya kuwa na msimu mzuri kwenye klabu aliyopelekwa kwa mkopo ya West Ham, Lingard amenza kwenye mchezo mmoja tu tokea Ralf Rangnick achukue majukumu ya kuinoa klabu hiyo.

Ralf Rangnick

“Kwa sasa akili yangu iko kwa wachezaji wote na kuweza kuwafahamu, tumekuwa pamoja kwa takribani wiki tatu, nahisi nina wafahamu vizuri wachezaji wote tulionao kwa sasa.

“Kwangu, nahitaji kuwaendeleza wachezaji wote lakini kama mchezaji anataka kuondoka kwasababu anahisi hatapata muda wa kutosha kucheza, tunaweza kuzungumza kuhusu hilo, lakini sio kuhusu mchezaji anachotaka, ni kuhusu hali ya klabu.

“Vitu viwili ambavyo vitatuweka pamoja ikiwa mchezeji anataka kuondoka, kitu cha kwanza ikiwa anataka kuondoka, lakini kingine ni mahitaji ya klabu inabidi yatimizwe.” Alisema Ralf Rangnick


KUWA MILIONEA MSIMU WA SIKUKUU NA SAHARA RICHIES

Unaanzaje siku yako katika msimu huu wa sikukuu, mchongo upo meridianbet kasino. Sloti pendwa ya Sahara Richies inaweza kukufanya ukawa milionea katika kufunga mwaka huu, Jiunge na ufurahie kasino maridhawa kutoka nyumba ya mabingwa.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.